Breaking

Sunday, 27 August 2023

WAJASIRIAMALI 100 WAHITIMU MAFUNZO YA SUPPLIER DEVELOPMENT PROGRAM YA STANBIC BIASHARA INCUBATOR

Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mussa Hassan Zungu (MB) akikabidhi cheti kwa mmoja wahitimu wa mafunzo ya mafunzo ya program ya Mpango wa Supplier Development Program yalioendeshwa chini ya kitengo cha Stanbic Biashara Incubator jijini Dar es salaam.

********

Na Samir Salum, Lango La Habari

Wajasiriamali 100 walioshiriki mafunzo ya program ya Supplier development inayoratibiwa na benki ya Stanbic chini ya mpango wa STANBIC Biashara Incubator wamehitimu na kutunukiwa vyeti na Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mussa Zungu.

Hafla ya kukabidhi vyeti kwa wahitimu imefanyika Agosti 26, 2023 katika ukumbi wa Kimataifa wa Mwalim Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es salaam ambapo Mh. Zungu amewapongeza Stanbic kwa mafunzo hayo huku akiwaasa wahitimu kuwa mabalozi wazuri wa program hiyo.

Mh. Zungu ameongeza kuwa Serikali ya jamhuri wa muungano wa Tanzania imejikita kuhakikisha kwamba watanzania wanafaidika na fursa na rasilimali zilizopo nchini na kupitia Mpango wa Tatu wa maendeleo FYDP III.

"tumejikita katika kukabiliana na changamoto zote zinazowakabili wajasiriamali na kuweka mifumo endelevu utakayowezesha kufikia malengo ya sera za Taifa za ushiriki wa watanzania (local content) katika kujenga uchumi" amesisitiza

Aidha ametoa rai kwa wahitimu kwenda kufanya kazi kwa mtazamo mpya wa kukabiliana na changamoto za jamii na kila mmoja wetu akatimize wajibu wake.

"Tukiwa ni kiungo muhimu katika kukuza uchumi wetu, kwa pamoja tunaweza kuleta mabadiliko, tunaweza kuinua jamii zinazotuzunguka na kuhakikisha tunakuwa na maendeleo jumuishi katika nchi yetu"
Kwa upande wake Meneja wa maendeleo ya Biashara Stanbic bwana Fred Max amesema mpango huo wa Stanbic Biashara Incubator sio programu tu bali ni kujitolea kwa hisani na kukuza mafanikio ya miradi ya ujasiriamali. Kupitia safu ya rasilimali na huduma za usaidizi wa biashara, tunalenga kuharakisha ukuaji wa kampuni hizi, tukiwapa zana wanazohitaji ili kustawi.


"Katika mpango huu kuna Vipengele ambavyo ni pamoja na anuwai ya rasilimali za usaidizi kama vile nafasi halisi, ujumuishaji wa mtaji, mafunzo na mwongozo, huduma za kawaida, na muhimu zaidi, ufikiaji wa mtandao muhimu wa miunganisho" ameeleza Bw. Max


Ameongeza kuwa kupitia mpango huo ambao umelenga kwa makampuni ya SME's ambayo yanachangia maendeleo ya kimkakati ya nchi yetu. Hasa, macho yetu yameelekezwa kwenye sekta ambazo zina jukumu muhimu katika ukuaji wa taifa letu ambazo ni Kilimo na Uzalishaji vifuniko vya ujenzi, kazi za kiraia, malighafi.


Amezitaja nyingine kuwa ni Usafiri, Upishi na Hotelier pamoja na wazalishaji wa Bidhaa za Watumiaji Zinazoenda Haraka (zinazojumuisha vifaa vya kuandikia, chakula, dawa, n.k.) pamoja na Huduma za Biashara ikiwa ni pamoja na sheria, elimu, fedha, kufundisha na Mawasiliano na Teknolojia


Akizingumzia lengo ya Mradi bwana Max amesema Malengo yetu ni wazi na yenye athari ambapo Stanbic Biashara Incubator imalenga kukuza Maudhui ya Ndani Kwa kuimarisha biashara za ndani na kunaziwezesha kupata kandarasi na kampuni za kimataifa, kuboresha ufikiaji wa uchumi wa ndani na athari kwa kiwango cha kimataifa pamoja na Kushughulikia Mahitaji ya Msururu wa Ugavi pia Kupitia mpango huu kukusanya taarifa.


Mwisho


Meneja wa maendeleo ya Biashara Stanbic bwana Fred Max Akifafanua jambo katika hafla ya wahitimu 100 wa mafunzo ya program ya Mpango wa Supplier Development Program yalioendeshwa chini ya kitengo cha Stanbic Biashara Incubator jijini Dar es salaam.






Naibu spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mbunge wa Jimbo la Ilala Mhe. Mussa Hassan Zungu akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ua wahitimu wa mafunzo ya program ya Mpango wa Supplier Development Program yaliondeshwa chini ya kitengo cha Stanbic Biashara Incubator katika hafla iliyofanyika jijini Dar es salaam

Bi Zakia Mohamed Mmoja wa wahitimu wa program ya supplier Development stanbic biashara incubator na kushinda tender baada ya kufanya mafunzo hayo na stanbic bank akielezea faida za zinazopatikana kupitia program hiyo.





Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages