Na Mwandishi Wetu
Mwanamuzuki Khaleed Ramadhan maarufu kama Tunda Man alifanya onyesho la aina yake kwenye shule ya Brilliant na kuzishauri shule ziwe na profamu za kuibua vipaji vya vijana.
Alitoa ushauri huo mwishoni mwa wiki wakati akitumbuiza kwenye mahafali ya shule ya sekondari ya Brilliant ya Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam.
Alisema mbali na masomo kuna umuhimu kwa shule kutenga muda wa michezo na burudani kwani kwa kufanya hivyo wataibua vipaji vingi na watu maarufu kwa siku za usoni.
Tunda Man aliibua shangwe kwa wanafunzi wa shule hiyo mara tu mshereheshaji wa tukio hilo alipotangaza uwepo wake kwenye mahafali hayo.
Aliposhuka kwenye gari lake wanafunzi walishindwa kujizuia na wote walivamia katikati ya uwanja na kuanza kuimba naye nyimbo mbalimbali ukiwemo ule wa naipenda Simba hatua uniue mimi sihami.
Tunda mbali na kuimba wimbo maarufu wa naipenda Simba sihami hata mniue aliimba nyimbo mbalimbali za kupongeza mafanikio ya timu ya Yanga hali iliyoibua furaha na shangwe kwa wanafunzi wa timu zote mbili.
Aliwataka wanafunzi wa shule hiyo wasome kwa bidii ili waweze kufanya vizuri kwenye mitihani yao ya kidato cha nne inayotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Mwanamuzuki Khaleed Ramadhan maarufu kama Tunda Man akiwapagawisha wanafunzi wa shule ya sekondari Brilliant wakati wa mahafali ya kidato cha nne ya shule hiyo yaliyofanyika shuleni hapo Mbezi Kimara kwa Msuguri jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.