Breaking

Thursday, 3 August 2023

TMDA YATOA TAULO ZA KIKE 1000 KWA WANAFUNZI URAMBO



Na Lucas Raphael,Tabora

Mamlaka ya dawa na vifaa tiba TMDA Mkoani Tabora wametoa taulo za kike pateki (1000) kwa ajili ya wanafunzi wa shule za sekondari wanaokutana na changamoto wawapo shuleni

makabidhiano hayo ya yamefanyika katika ofisi ya mbunge wa jimbo la urambo mkoani hapa Margaret Sita ambaye alisema kumekuwa na uhitaji mkubwa wa taulo za kike kwa wanafunzi wa shule za Sekondari na msingi .

Alisema kwamba taulo hizo zitaenda kuwanufaisha wanafunzi wa shule mbalimbali kama itakavyoratibiwa kwa kuangalia vigezo vya shule zenye uhitaji zaidi

"Tumekuwa na uhitaji wa taulo za kike japokuwa tumeendelea kupambana na changamoto hiyo kwa kuleta taulo za kike mara kwa mara na wakati mwingine tunawafundisha wanafunzi kujitengenezea taulo za kienyeji ambazo nazo huwafaa lakini kwa ujio wenu TMDA kumeleta tija kubwa kwetu" Alisema Margaret Sita

kwa upande wake kaimu afisa elimu wa shule za Sekondari wilayani urambo Rudia Masatu alikili changamoto zinazowakuta wanafunzi wa jinsi ya kike ambao wengi wao hulazimika kusitisha baadhi ya vipindi darasani wanapoingia kwenye siku zao hivyo ameshukuru na kumpongeza mbunge kwa kuwaleta wageni hao.

Meneja wa mamlaka ya dawa na vifaa tiba TMDA kanda ya magharibi Christopher Migoha aliwataka madiwani kuiga mfano huo kwa kuwawezesha wanafunzi waliopo kwenye shule za Sekondari zilizopo kwenye kata zao ili kuwasaidia katika changamoto ya kukatisha masomo yao.

"Madiwani mliopo hapa jifunzeni kitu kutoka kwetu angalieni uhitaji uliopo kwenye kata zenu pia wawezesheni watoto wa jinsi ya kike wao wanakabiliwa na changamoto kubwa kwa hiyo jitahidini kuwapa taulo za kike" alisema Christopher Migoha

Naye katibu wa chama cha mapinduzi ccm wilaya ya urambo Himid Tweve na madiwani wa kata za kapilula Paulo Shija na kiyungi Ahmed Seif walishiriki makabidhiano hayo wakisema agizo la walilopewa wataenda kulitekeleza.

mwisho
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages