Breaking

Wednesday, 2 August 2023

TBS YASHIRIKI MAONESHO YA NANE NANE KANDA YA KUSINI

NA MWANDISHI WETU

SHIRIKA la Viwango Tanzania (TBS) kanda ya Kusini, limeendelea kutoa elimu ya Viwango vya Ubora kwa wazalishaji, wauzaji na waigizaji wa bidhaa kwenye Maonesho ya Nane Nane yanayoendeleo kwenye viwanja vya Ngongo mkoani Lindi.

Akizungumza kwenye Maonesho hayo leo Augost 2, 2023 Meneja wa Kanda ya Kusini, Mhandisi Saidi Mkwawa amesema kumekuwa na uingizaji wa bidhaa nchini ambavyo havina viwango, hivyo kupitia maonesho hayo wanatumia kuelimisha wananchi kuhusu masuala ya viwango.

Aidha amewataka wazalishaji wa bidhaa kufika kwenye banda la TBS lililopo kwenye Maonesho hayo ili waweze kupatiwa elimu ya namna bora ya uzalishaji pamoja na kufanya usajili wa majengo ya chakula na vipodozi.

Amesema kupitia Maonesho hayo imekuwa ni rahisi kuwafikia wajasiriamali mbalimbali wanaotembelea maonesho hayo kuwapatia elimu kuhusu masuala ya viwango wakati wanapozalisha na kuuza bidhaa zao.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages