Breaking

Wednesday, 16 August 2023

RAIS MWINYI AIPONGEZA DAWASA KUSHIRIKI KONGAMANO LA MAJI ZANZIBAR 2023

Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imeshiriki kwenye kongamano la utekelezaji wa programu ya uwekezaji kwenye sekta ya Maji Zanzibar (Zanzibar water investment programme).

Programu hiyo ilizinduliwa Mwaka 2022 kwa kuweka banda la kuonyesha utekelezaji wa mipango mbalimbali ya mamlaka pamoja na mafanikio ya sekta ya maji katika Mkoa wa Dar es Salaam, Pwani na baadhi ya maeneo ya Tanga na Morogoro.

Kongamano hilo limeandaliwa na Wizara ya Maji, Nishati na Madini ya Zanzibar kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya maji ambapo Mgeni Rasmi ni Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza Dk. Hussein Ali Mwinyi.

Lengo la kongamano hilo ni kukukitanisha wadau wa maji, kujadili na kubadilishiana uzoefu katika masuala mbalimbali pamoja na kutambua maeneo ya ushirikiano ambapo kauli mbio ya kongamano hilo ni "Kuongeza kasi ya mabadiliko: katika kufikia usimamizi endelevu wa Rasilimali za maji chini ya ardhi pamoja na uhimilivu kwa kwa wote".

Katika kongamano hilo Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Ali Mwinyi ameitaka Wizara ya Maji Zanzibar kuimarisha huduma ya Usambazaji wa Maji na Usafi wa Mazingira kupitia ubunifu na teknolojia ya kisasa na miundombinu (Enhancing water supply na Sanitation through innovative and climate-smart technologies and infrastructures) pamoja uimarishaji wa tasisi za usimamizi wa maji.

"Nianze kwa kumshukuru Mungu kwa kuweza kutupa uhai na kukutana leo hapa katika kongamano la pili ambalo lilianzishwa mwaka jana kama mnavoelewa sekta ya maji ni muhimu kwa viumbe hai na mimea" amesema Dk. Mwinyi.

"Kama mnavyoelewa tafiti nyingi zimefanyika na katika maeneo ya Unguja na pemba na kubaini vyanzo vya maji chini ya ardhi vinavyo ridhisha hivyo na agiza wizara ya maji Maji, Nishati na Madini Zanzibar kuendelea kufanya kazi kwa karibu na wataalum mbalimbali wa sekta ya maji na kuandaa mpango maalum wa maji yaani "Water master plan" alisema Dk. Mwinyi.

DAWASA ikiwa ni mmoja wa washiriki katika kongamano hilo imepata fursa kutoa elimu ya huduma ya maji pamoja na kuelezea mafanikio ya sekta ya maji katika jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani pamoja na baadhi ya maeneo ya Morogoro na Tanga kupitia kutekeleza miradi ya kimkakati.

Akizungumza Meneja wa Usambazaji maji DAWASA Mhandisi Tyson Mkindi wakati Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Mwinyi alipotembelea banda la DAWASA ameeleza kuwa Mamlaka imejipanga kufikia asilimia 95% ya upatikanaji wa huduma ya maji katika eneo lake la kihuduma pamoja na kupunguza kiwango cha upotevu wa maji kupitia uboreshaji wa huduma wa TEHAMA.
" Serikali imeelekeza kufikia mwaka 2025 tufikie asilimia 95 na Mamlaka imejipanga kutekeleza miradi ya kimkakati haswa maeneo ya pembezoni yaliyokuwa bado ili kufikia malengo hayo" alisema Mhandisi Mkindi.
Rais wa Serikali wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt Hussein Ali Mwinyi akipata maelezo kutoka kwa Meneja wa Usambazaji maji Mhandisi Tyson Mkindi alipotembelea banda la Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) ambapo aliambatana Katibu Mkuu Kiongozi wa serikali ya Zanzibar Mhandisi Zena Saidi (wa kwanza kulia), Waziri wa Maji Zanzibar Mhe. Shaibu Kaduwara (wa pili kulia) na Naibu Waziri wa Maji serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Mhandisi Maryprisca Mahundi (wa tatu kulia).

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages