Naibu Waziri wa Maji, Mheshimiwa Mhandisi Maryprisca Mahundi amewasili kwenye Ofisi za DAWASA zilizopo Mwananyamala na kupokea taarifa ya hali ya Upatikanaji wa huduma ya maji katika Mkoa wa Dar es Salaam kutoka kwa Kaimu Mtendaji wa DAWASA Mhandisi Shabani Mkwanywe baada ya hapo ataanza Ziara ya Siku tatu kwa kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya maji.
Pia, wakati wa kupokea taarifa hiyo Mhe. Mahundi ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe. Saad Mtambuli.