Breaking

Thursday, 3 August 2023

MSITUMIE FEDHA ZA MIKOPO KUNUNULIA MADERA - ANNE MAKINDA

 


Anne Makinda

 Na Rose Mwalongo - Dar es salaam
Wanawake nchini wameaswa kutumia mikopo wanayopewa kwa kile kilichokusudiwa na sio kununua madera au kwa kitchen parties kwani bila hivyo watashindwa kurejesha.

Wito huo ulitolewa hivi karibuni na Bi. Anne Makinda, Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania wakati wa maadhimisho ya Siku ya Wanawake Afrika ambayo yaliandaliwa na WILDAF pamoja na Women Think Tank jijini Dar es Salaam.

Alisema wakati wa sensa ya watu na makazi waligundua kuwa kaya nyingi zinaendeshwa na wanawake na hivyo akawashauri kuwa makini kwani baadhi wamekuwa wakitumia mikopo kwa mambo ya kijamii na wanaposhindwa kurejesha huishia kujitoa uhai.

Maadhimisho hayo yaliambatana na kutambua Mchango wa Marehemu Sheikh katika kutetea haki za wanawake Tanzania.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages