Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora, Richard Abwao |
Mwanamke mmoja mkazi wa Kata ya Itobo wilayani Nzega anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani Tabora kwa tuhuma za kuwanywesha sumu watoto wawili wa mume wake na kusababisha vifo vyao.
Watoto hao ambao wamefahamika kwa majina ya Dickson Zakaria aliyekuwa na miaka mitano ( 5) na Godluck Zakaria aliyekuwa na minne (4).
Akithibitisha kutokea kwa vifo hivyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Richard Abwao amesema mwanamke huyo ambaye jina lake limehifadhiwa mnamo tarehe 12 August 2023 majira ya usiku anadaiwa kuwanywesha sumu watoto hao wawili wa kambo baada ya kugombana na mumewe nakumalizia hasira zake kwa watoto hao kwa kuwanywesha sumu aina ya Super feed NPK na Bens Attack 344 SE ambayo ni dawa ya kuulia wadudu kwenye mazao na kisha naye kunywa sumu hiyo hali iliyosababisha kupoteza fahamu na kukimbizwa hospitali.
Kwa mujibu wa Kamanda Abwao mtuhumiwa amekiri kutenda kosa hilo akidai mumewe amewatelekeza na amekuwa hampatii pesa za matumizi ya familia huku naye akiwa ana ujauzito.
chanzo:Azam tv