Breaking

Sunday, 27 August 2023

KUNDO AZUNGUMZA NA WAKUU WA MIKOA NA MAKATIBU TAWALA KIBAHA

Na Grace Semfuko- MAELEZO

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew amezungumza na Wakuu wa Mikoa ambapo amesema zoezi la mfumo wa anwani za makazi limevuka lengo kwa kuongezeka kwa asilimia 12.8 ya matarajio ya awali ya asilimia mia moja na kuwaomba Wakuu hao kuendelea kulisimamia zoezi hilo endelevu.
Amesema kuna Mabadiliko Makubwa yaliyotokea kufuatia utekelezaji wa mfumo huo ambayo ni pamoja na Wananchi kupata faida nyingi kwa urahisi ikiwepo ya kupata, kutoa, kupokea na kufikisha huduma mahali stahiki na kwa wakati.

Alizungumza wakati akitoa mada kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala nchini waliokuwa kwenye mafunzo Kibaha Mkoani Pwani, Mhandisi Kundo amesema ipo haja ya Wakuu hao kusimamia na kulifanya zoezi hilo kuwa endelevu.

Lakini kwa sababu haya yote yanafanyika katika Halmashauri, Wilaya na Mikoa, ni muhimu kwenu kuendelea kutusaidia katika Halmashauri mnazozisimamia kuhakikisha kuna fedha inayoendelea kutengwa kwa ajili kufanya zoezi hili liwe endelevu na faida kwa wananchi. Amesema Mhandisi Kundo.

Amezitaja sababu zinazolifanya zoezi hilo kuwa endelevu ni pamoja na kuongezeka kwa idadi ya Maendeleo ikiwepo watu na ujenzi wa miundombinu.

Sasa mtu anaweza akajiuliza kwanini kama tumemaliza hili zoezi kwa nini tunaendelea tena, mfumo wa anwani za makazi ni sehemu ya maisha ya Watanzania, ni sehemu ya maisha ya watu wote Duniani, tunapojenga barabara, tunapojenga nyumba, watu wanapozaliwa kunakuwa na mabadiliko ambayo ni lazima iwe na mkakati uendelezaji wa zoezi hili. Amesema Mhandisi Kundo.

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew akizungumza wakati akitoa mada kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala nchini waliokuwa kwenye mafunzo jana Agosti 26,2023 Kibaha Mkoani Pwani,
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew akizungumza wakati akitoa mada kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala nchini waliokuwa kwenye mafunzo jana Agosti 26,2023 Kibaha Mkoani Pwani,
Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew akisisitiza jambo wakati akitoa mada kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala nchini waliokuwa kwenye mafunzo jana Agosti 26,2023 Kibaha Mkoani Pwani,

Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew akitoa mada kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala nchini waliokuwa kwenye mafunzo jana Agosti 26,2023 Kibaha Mkoani Pwani,
Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala wakimsikiliza Naibu Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhandisi Kundo Mathew akitoa mada kwa viongozi hao kwenye mafunzo kwa Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala jana Agosti 26,2023 Kibaha Mkoani Pwani,

Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa,Mheshimiwa Innocent Bashungwa akiwa kwenye Mafunzo ya Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala jana Agosti 26,2023 Kibaha Mkoani Pwani,
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages