Breaking

Wednesday, 30 August 2023

JAMII YATAKIWA KUWAPA NAFASI WANAWAKE KWENYE UONGOZI

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

JAMII imetakiwa kuachana na imani potofu zinazomkandamiza mwanamke ili chaguzi zijazo, wanawake wengi wajitokeze kwa wingi katika kugombea uongozi kwenye nafasi mbalimbali kwani uwepo wao kwenye uongozi inaleta chachu ya maendeleo kwenye jamii.
Ushauri huo umetolewa leo Agosti 30,2023 katika Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) ambapo walikuwa wanajadili nafasi ya mwanamke katika ushiriki kwenye uongozi.

Akizungumza wakati akiwasilisha mada, mwezeshaji Bi. Clara Mcharo amesema kuwa jamii imekuwa haina imani na wanawake katika uongozi kutokana na tamaduni zilizopo kwenye jamii ambazo zinaamini kuwa mwanamke hawezi kuwa kiongozi.

Amesema iwapo dini zetu zikiwashirikisha wanawake katika uongozi basi jamii pia itapata uelewa mkubwa katika kuamini wanawake wanaweza hivyo kuwapa nafasi kwenye uongozi ili kuonesha uwezo wao.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages