NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
KUELEKEA Dira ya Maendeleo ya mwaka 2025-2050, wananchi wameishauri Serikali kuhakikisha inawashirikisha katika kila jambo ambalo lotakuwa na manufaa kwa nchi ili kuondokana na migogoro baina ya Serikali na Wananchi.
Akizungumza leo Augosti 9,2023 Jijini Dar es Salaamwakati wa Semina za Jinsia na Maendeleo zinazoendeshwa na Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Bw. Venancy Peter amesema ushirikishwaji wa wananchi utsaidia kuondoa migogoro ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara baina ya Serikali na wananchi hasa kwenye masuala ya kiuchumi.
"Tunatumaini Dira ya Maendeleo ijayo ya mwaka 2025 kuelekea 2050 kuona kwamba jamii sasa ishirikishwe kwa kila jambo lenye manufaa kwa taifa letu". Amesema
Kwa upande wake Mshiriki wa Semina, Bi.Subira Abdalah amesema Serikali ijaribu kuzungumza na wananchi kile ambacho wamekiona ili kutengeneza taifa lenye manufaa hapo baadae.