WILAYA ya Rungwe mkoani Mbeya imemshukuru Rais Dk.Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kufanikisha mapambano ya vifo vitokanavyo na uzazi pingamizi, ambapo katika hospitali ya wilaya wanawake zaidi ya 350 wanajifungua kwa mwezi wakiwa salama na watoto.
Uongozi wa wilaya hiyo akiwemo Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Suma Fyandomo, amesema katika mapambano hayo ya vifo vitokanavyo na uzazi wanamtambua Rais Samia kama askari namba moja mkoani humo kutokana na uimarishaji wa huduma za afya ikiwemo upatikanaji wa uhakika wa vifaa.
Akizungumza jana katika hospitali ya Wilaya ya Rungwe mkoani humo Suma amesema wanamshukuru Rais Dk.Samia kwa kuendelea kufanikisha mapambano ya vifo vitokanavyo na uzazi pingamizi ambapo katika hospitali ya wilaya wanawake zaidi ya 350 wanajifungua kwa mwezi wakiwa salama wao na watoto.
Alisema katika mapambano hayo wanamtambua Rais Dk.Samia kama shujaa na askari namba moja aliyedhamilia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi nchini.
“Mkoa huu ni kati ya mikoa ambayo watu wanazaliana kwa wingi na hapo awali huduma za afya hususani za uzazi zilikuwa ni changamoto katika vituo na hospitali zetu lakini kwa sasa hususani miaka miwili hii ya Rais Dk.Samia tumeona uthubutu na uchungu alionao kwa wanawake wenzie ambapo vifaa tiba na mazingira wezeshe ya klujifungulia yanatuma uhakika wa kuwapo kwa uzazi salama,”alisema.
Suma alieleza kuwa,katika hospitali hiyo wanajifungua wanawake zaidi ya 350 kwa mwezi na wote wanakuwa salama na watoto.
Alisema, kwa namna ambavyo uongozi wa Rais Dk.Samia unamjali mama na motto maboresho ya wodi za kujifunmgua yamezingatia upatikanaji wa vifaa vyote vya afya vya kisasa kutoka Bohari ya Dawa (MSD) katika vituo vyote hadi vya pembezoni ambapo kwa sasa wanafanya upasuaji.
“Kuanzia Kyela,Chunya, Mbaral, Mbeya mjini na Vijijini hakuna maha;li kuna malalamiko ya kukosa dawa na vifaa tiba hadi ngazi ya zahanati kuna majengo ya kisasa ikiwemo ya huduma za dharula ambapo ujezi unaendelea kila sehemu , nami katika kuunga mkono jitihada hizo nimenunua mashuka, viti mwendo kutoka MSD,”alisema.
Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Halmashauri Wilaya ya Rungwe Dk.Diocles Ngaiza alisema katika idara ya afya maboresho yamekuwa yakiendelea ambapo mwaka 202/23 na kufungua vituo vya afya viwili vya Ndanto na Kyimo ambavyo vimepokea mil. 500 kila kimoja na vimeanza kutoa huduma vikiwa na vipaumbele ya huduma ya afya na mama na mtoto kwa maelekezo ya Rais Samia na serikali yake lengo ni kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi wilayani humo.
“Pia vipo vituo vya afya vingine viwili vinaendelea kujengwa kikiwemo cha Iponjora ambapo tulipokea milioni 500 ujenzi upo katika hatua za mwisho na kituo cha Kinyala ujenzi unaendelea kwa fedha za mapato ya ndani vyote vimelenga kuboresha huduma ya mama na moto,”alisema.
Dk.Ngaiza alisisitiza kuwa,mbali na maboresho hayo ujenzi wa ghorofa unaendelea katika hospitali ya wilaya ambapo wamepokea sh bilioni moja kwa mwaka wa fedha uliopita na matarajio ni kupata bilioni moja nyingine kutoa wizarani kuweza kukamilisha ujenzi huo ambao utahusisha wodi za wagonjkwa wan nje,wa ndani, wodi za mama na mtoto.
Alisema upande wa vifaa tiba kwa mwaka wa 2022/23 wamepokea sh. milioni 400 kwa ajili ya vifaa tiba ambavyo vimefungwa katika vituo na huduma zinaendelea huku katika bajeti ya mwaka huu idara ya afya imetenmgewa sh . bilioni 2.8 zitakazonunua vifaa tiba vya sh. milioni 700 na bilioni moja nyingine ya ujenzi wa vituo vipya viwili vya afya.
“Kipekee idara ya afya imepewa kipaumbele tunaishukuru serikali ya awamu ya sita na Bohari yetu kwa kuwa hizi dawa na vifaa tiba vyote vinatoka MSD na upatikanaji wa dawa katika wilaya hii ni asilimia 92, nishukuru sana uongozi wa taasisi hiyo Mbeya hivi karibuni nilipeleka ombi la kupatiwa mashine kubwa ya dawa ya usingizi ilikuwa haipo walipambana imefika hivyo muda wowote tutaanzisha upasuaji katika kituo cha afya cha Kimo,”alisema.