Breaking

Thursday, 13 July 2023

WAZIRI MABULA ASHIRIKI MKUTANO WA KAMISHENI YA BONDE LA MTO SONGWE

Na Munir Shemweta, WANMM

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula ameshiriki Mkutano wa Pili wa Baraza la Mawaziri wa Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe uliofanyika leo tarehe 13 Julai 2023 Jijini Dar es Salaam.

Mkutano huo wa siku moja unaoongozwa na Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Awesu unahusisha viongozi na wataalamu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na Malawi huku ujumbe wa Malawi ukioongozwa na Waziri wake wa Maji na Usafi wa Mazingira Mhe. Abida Sidik Mia

Mawaziri wengine wa Tanzania wanaoshiriki mkutano huo ni Mhe. Anthony Mavunde, Naibu Waziri wa Kilimo, Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Deogratius Ndejembi na Naibu Waziri wa Nishati Mhe. Stephen Byabato.

Mkutano huo ni muendelezo wa vikao vya pamoja baina ya Serikali ya Tanzania na Malawi unaolenga kuimarisha usimamizi, uhifadhi, uendelezaji na matumizi endelevu ya rasilimali ya maji ya mto Songwe.

Tanzania na Malawi zilishiriki majadiliano ya pamoja yaliyofanyika mwaka 1976 kuhusu namna bora ya kutatua changamoto zinazosababishwa na Mto Songwe kwa madhumuni ya kutafuta ufumbuzi wa kudumu.
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. Dkt Angeline Mabula (kulia) akiwa na Mawaziri wenzake Anthony Mavunde, Naibu Waziri wa Kilimo na Deogratius Ndejembi Naibu Waziri TAMISEMIA katika Mkutano wa Pili wa Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe unaofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 13 Julai 2023.
Sehemu ya washiriki wa mkutano wa Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe unaofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 13 Julai 2023.
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Awesu (Kushoto) akiwa na Waziri wa Maji wa Malawi M Abida Sidik Mia katika mkutano wa pili wa Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe unaofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 13 Julai 2023.
Ujumbe wa Malawi ukiwa katika Mkutano wa Pili wa Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe unaofanyika jijini Dar es Salaam tarehe 13 Julai 2023. (PICHA NA WIZARA YA ARDHI)

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages