Breaking

Wednesday, 26 July 2023

WAWILI WAKAMATWA WAKIDAIWA KUTOROSHA MADINI




Jeshi la Polisi Mkoa wa Morogoro linawashikilia watu wawili ambao ni Jackson Peter Mtangi (35) pamoja na Jafari Fanikiwa Siwelo (29) wanaotuhumiwa kutorosha madini.

Kupitia taarifa iliyotolewa leo na Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro ACP Hassan Maya amesema kuwa watuhumiwa hao walikamatwa Julai 25, 2023 wakiwa na viroba 8 vya mawe na viroba 24 vya mchanga vinavodhaniwa ni madini.

Amesema watuhumiwa hao ambao ni wakazi wa Chinangali Dodoma walikuwa wakisafirisha madini hayo kwa kutumia gari lenye namba za usajili T.376 AQL aina ya Toyota Tandcruiser rangi nyeupe ambayo ni mali ya kampuni ya Shelabichi tours iliyopo Dar es salaam katika barabara itakayo Morogoro kwenda Dodoma.

"Baada ya mahojiano watuhumiwa walieleza kuwa madini hayo wameyatoa kwa mtu waliomtaja kwa jina moja la Luka aliyepo kitongoji cha lbondo kijiji cha Mtega kata ya Chanjale tarafa ya Nongwe wilaya ya Gairo" ameeleza Kamanda Maya
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages