Breaking

Saturday, 22 July 2023

WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA, MWANZA NA SIMIYU WAPEWA MAFUNZO YA CHANJO

Afisa Mpango wa Taifa wa Chanjo - Wizara ya Afya, Lotalis Gadau akizungumza wakati wa mafunzo ya Chanjo kwa Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga, Mwanza na Simiyu
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Claudia Kaluli ambaye ni Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akifungua mafunzo ya Chanjo kwa Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga, Mwanza na Simiyu

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Wizara ya Afya imetoa Mafunzo kuhusu masuala ya chanjo mbalimbali kwa Waandishi wa habari Mikoa wa Shinyanga, Mwanza na Simiyu yenye lengo la kuhamasisha watu kupata chanjo hususan watoto chini ya miaka mitano.

Akifungua mafunzo hayo ya siku moja yaliyofanyika leo Jumamosi Julai 22,2023 Jijini Mwanza, Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Claudia Kaluli ambaye ni Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza amesema waandishi wa habari wamekuwa msaada mkubwa katika kuelimisha wananchi juu ya magonjwa na chanjo hivyo kuwaomba waendelee kuwahamasisha wananchi kuhusiana na chanjo kwani wananchi wana imani na vyombo vya habari.

“Mafunzo haya yanalenga kuwajengea uwezo waandishi wa habari kuhusu masuala ya chanjo mbalimbali. Tunawashukuru Wanahabari mnatusaidia sana kuelimisha wananchi kuhusu masuala ya chanjo”,amesema.

Naye, Afisa Mpango wa Taifa wa Chanjo - Wizara ya Afya, Lotalis Gadau amezitaja miongoni mwa chanjo zinazotolewa nchini Tanzania kwa wajawazito,mabinti pamoja na watoto chini ya miaka mitano ikowemo chanjo ya UVIKO - 19, Kifua Kikuu (BCG),Polio (OPV), Polio (IPV), Surua Rubela (MR), (Donda koo, kifaduro,pepo punda, homa ya Ini homa ya uti wa mgongo, homa ya mapafu -Pentavalent), Pepo punda, Saratani ya Mlango wa Kizazi (HPV), Nimonia (PCV13) na Kuhara Kukali ( Rota).

Gadau amesema hali si shwari kwa saratani ya mlango wa kizazi hivyo amewataka akina mama kujenga mazoea ya kupima saratani ya mlango wa kizazi ili kuchukua hatua mapema.

Amesema Wizara ya Afya imekuwa ikitoa mafunzo ya chanjo kwa waandishi wa habari maeneo mbalimbali nchini ili kuhakikisha waandishi wa habari wawe na uelewa unaofanana kuhusu masuala ya chanjo.

“Naomba mkawe mabalozi wa kuelimisha jamii, kanusheni uvumi au uzushi unaojitokeza na chanjo iwe ajenda katika fursa yoyote ipatikanayo”,amesema Gadau.

Kwa upande wake, mratibu wa chanjo Mkoa wa Mwanza Amos Kiteleja amewasihi wananchi wafike hospitali kupata chanjo ya homa ya Ini kwani ni ugonjwa hatari.

Naye Mhamasishaji Chanjo kutoka Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar , Ruzuna Abdulrahim Mohammed amewasisitiza akina mama kunyonyesha watoto wao mara tu baada ya kujifungua ili kuhakikisha watoto wanakuwa na afya njema.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Claudia Kaluli ambaye ni Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akifungua mafunzo ya Chanjo kwa Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga, Mwanza na Simiyu leo Jumamosi Julai 22,2023 katika Ukumbi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Claudia Kaluli ambaye ni Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akifungua mafunzo ya Chanjo kwa Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga, Mwanza na Simiyu
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Claudia Kaluli ambaye ni Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akifungua mafunzo ya Chanjo kwa Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga, Mwanza na Simiyu
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Claudia Kaluli ambaye ni Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akifungua mafunzo ya Chanjo kwa Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga, Mwanza na Simiyu
Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Claudia Kaluli ambaye ni Muuguzi Mkuu wa Mkoa wa Mwanza akifungua mafunzo ya Chanjo kwa Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga, Mwanza na Simiyu
Afisa Mpango wa Taifa wa Chanjo - Wizara ya Afya, Lotalis Gadau akizungumza wakati wa mafunzo ya Chanjo kwa Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga, Mwanza na Simiyu
Afisa Mpango wa Taifa wa Chanjo - Wizara ya Afya, Lotalis Gadau akizungumza wakati wa mafunzo ya Chanjo kwa Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga, Mwanza na Simiyu
Mratibu wa chanjo Mkoa wa Mwanza Amos Kiteleja akizungumza wakati wa mafunzo ya Chanjo kwa Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga, Mwanza na Simiyu

Mhamasishaji Chanjo Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar , Ruzuna Abdulrahim Mohammed akizungumza wakati wa mafunzo ya Chanjo kwa Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga, Mwanza na Simiyu

Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - Wizara ya Afya, Catherine Sungura akizungumza wakati wa mafunzo ya Chanjo kwa Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga, Mwanza na Simiyu

Mwenyekiti wa mafunzo, Belensi China akizungumza wakati wa mafunzo ya Chanjo kwa Waandishi wa habari Mkoa wa Shinyanga, Mwanza na Simiyu
Waandishi wa habari wakiwa kwenye mafunzo ya Chanjo

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages