Breaking

Monday, 17 July 2023

TUME YA BONDE LA MTO SONGWE YAPATA BOSI MPYA

BARAZA la mawaziri la bonde la mto Songwe limemteua Mhandisi Dk Ladislaus Kyaruzi Leonidas kuwa Katibu Mtendaji mpya wa kwanza wa Tume ya Pamoja ya Bonde la Mto Songwe (SONGWECOM).

Tume ya bonde la mto Songwe inaundwa kwa pamoja na Serikali za Tanzania na Malawi ambapo mwaka 2019 Tanzania na Malawi zilizindua tume ya pamoja kwenye Bonde la Mto Songwe kwa lengo la kuendesha miradi ya umwagiliaji na uzalishaji wa umeme yenye thamani ya dola za Kimarekani milioni 829.

Dk Kyaruzi ambaye ni Mhandisi na mwenye Shahada ya Uzamivu katika Mabadiliko ya Tabia nchi na Maendeleo Endelevu katika Chuo Kikuu cha Dar es salaam (UDSM) ameanza majukumu yake tangu Julai 1, 2023, baada ya kuchukua nafasi ya Bw. Hyde R.G. Sibande aliyekuwa akiKaimu nafasi Katibu Mtendaji wa bonde hilo.

Kabla ya uteuzi wake mpya, Dk Kyaruzi alikuwa Mkuu wa Sekretarieti ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) anayehusika na mazingira na maliasili .

Mwaka 2011-2021, alikuwa amehudumu kama mpatanishi wa kikundi cha Kiafrika kinachojadiliana juu ya mabadiliko ya hali ya hewa kwa mchakato wa UNFCCC .

Dk Kyaruzi pia ni mjumbe wa Kamati tendaji ya teknolojia ya ulimwenguni kwenye mkataba wa mfumo wa umoja wa mataifa wa mabadiliko ya tabianchi (2018 hadi sasa).

Dk Kyaruzi pia ni amesaidia kuratibu marekebisho ya Itifaki ya jumuiya ya usimamizi wa mazingira na maliasili katika jumuiya ya Afrika Mashariki.

Pia aliratibu uendelezaji wa Mkakati wa Kitaifa wa mabadiliko ya tabia nchi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa upande wa uongozi na uhusiano na mashirika au taasisi zinazofanana za kikanda na kimataifa, kuanzia Dr 2016-2017, Dr Kyaruzi alikuwa Mwenyekiti wa tawi la uwezeshaji Duniani la Kamati ya ufuatiliaji ya Itifaki ya Kyoto kwa mkataba wa umoja wa mataifa wa mabadiliko ya tabianchi (Global Facilitative Branch of the Compliance Committee of the Kyoto Protocol to the United Nations Framework Convention on Climate Change).

Lakini pia Dr Kyaruzi aliwahi kuwa Makamu mwenyekiti wa tawi la uwezeshaji duniani la kamati ya ufuatiliaji ya Itifaki ya Kyoto tangu 2014 hadi 2015.

Vilevile kwa mwaka 2013-2014 alikuwa Mjumbe wa timu ya wataalamu kutoka Tanzania kwa Mratibu wa Kamati ya Wakuu wa Nchi na Serikali za Afrika kuhusu Mabadiliko ya tabia nchi (the Coordinator of the Committee of African Heads of State and Government on Climate Change (CAHOSCC)) wakati Tanzania iliporatibu CAHOSCC.

Kwa upande wake, Waziri wa Maji , Mheshimiwa Jumaa Aweso (Mb) amempongeza Dk Kyaruzi kwa kuteuliwa na kuongeza kuwa ana imani kuwa, tume ya bonge la mto Songwe iko mikononi katika mikono salama.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages