Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli (PURA) imenogesha maonesho ya Saba Saba 2023 kwa kuja na kifaa maalumu kinachoonesha uhalisia tepe (virtual reality) wa namna mradi wa kusindika gesi asilia (Liquefied Natural Gas - LNG) utakavyokuwa.
Mradi wa LNG unalenga kuendeleza gesi asilia iliyogundulika katika kina kirefu cha bahari na mitambo ya kuchakata na kusindika gesi hiyo itajengwa katika eneo la Likong'o Mkoani Lindi.
Baadhi ya wananchi waliotumia kifaa hicho wameeleza kufurahishwa na ubunifu uliotumika na kuipongeza PURA kwa kuwaletea mradi huo katika uhalisia kwa kuwa imewafanya wauelewe zaidi, tofauti na kutoa maelezo bila kuona uhalisia tepe.
Mmoja wa wananchi aliyetembelea banda la PURA akitumia kifaa cha uhalisia tepe kuangalia namna mradi wa LNG utakavyokuwa