Makundi mbalimbali ya wananchi wanaotembelea maonesho ya 47 ya Saba Saba yaliyoanza tarehe 28 Juni, 2023 wameendelea kumiminika kwenye banda la Mamlaka ya Udhibiti Mkondo wa Juu wa Petroli kupata uelewa wa masuala ya utafutaji na uzalishaji wa gesi asilia nchini.
Pamoja na kutoa elimu hiyo, PURA pia inaelezea majukumu inayoyatekeleza kwa mjibu wa Sheria ya Petroli ya mwaka 2015 yakiwemo kuishauri Serikali juu ya masuala ya mkondo wa juu wa petroli; kusimamia na kudhibiti shughuli za mkondo wa juu wa petroli; na kuhamasisha ushiriki wa Watanzania katika miradi ya mafuta na gesi asilia inayotekelezwa nchini.
Mha. Ndau Ndau kutoka PURA (Kushoto) akitoa maelezo kwa mmoja wa wananchi waliotembelea banda la PURA katika maonesho ya Saba Saba 2023 yanayoendelea Jijini Dar es Salaam
Bw. Hakeem Mwaruka kutoka PURA akitoa maelezo kwa baadhi ya wananchi waliofika banda la PURA katika maonesho ya 47 ya Saba Saba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam.