Breaking

Thursday, 13 July 2023

NIT KUENDELEA KUIBUA WATAALAMU KWENYE SEKTA YA ANGA NCHINI

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Franklin Rwezimula amefanya ziara na kukagua Maendeleo ya Mradi wa Kituo Cha Umahiri katika Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) ambapo amekagua majengo, mitambo na vifaa mbalimbali vya kufundishia wanafunzi Masuala ya ndege ikiwemo Marubani,Wahandisi na wahudumu ndani ya ndege.

Akizungumza mara baada ya kufanya ukaguzi huo leo Julai 13,2023 Jijini Dar es Salaam, Dkt.Rwezimula amesema taifa linakabiliwa na uhaba wa Wataalamu katika sekta ya usafiri wa anga hivyo kuanza kutolewa kwa kozi ya Masuala ya ndege katika chuo hicho, kitasaidia kuwa na wataalam wa kutosha.

"Kukamilika kwa mradi huu kutasaidia sana kuzalisha wataalamu wa kutosha katika sekta ya usafirishaji lakini pia chuo hiki kitakuwa na uwezo wa kupokea Wanafunzi wengi zaidi kutoka nje ya nchi". Amesema

Aidha Dkt.Rwezimula amekipongeza Chuo hicho kwa kutekeleza mikakati mikubwa katika kuhakikisha sekta ya usafairishaji inakua kwa kiasi kikubwa hapa nchini hasa katika kuhakikisha wanazalisha wanataaluma bora kwenye sekta hiyo.

Nae Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa amesema kwa sasa mradi huo upo katika hatua mbalimbali za Ujenzi na kwamba mwishoni mwa mwaka 2024 mradi huo utakuwa umekamilika.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Franklin Rwezimula akimsikiliza Msimamizi wa Mradi Mhandisi Juma ngoda wakati alipofanya ziara na kukagua Maendeleo ya Mradi wa Kituo Cha Umahiri katika Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT)leo Julai 13,2023 Jijini Dar es Salaam

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Franklin Rwezimula akiwa kwenye chucha cha kufundishia wanafunzi NIT wakati alipofanya ziara na kukagua Maendeleo ya Mradi wa Kituo Cha Umahiri katika Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT)leo Julai 13,2023 Jijini Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Franklin Rwezimula akimsikiliza Afisa Viwango na Usalama kazini NIT, Mhandisi Ahmed Mwinge wakati alipofanya ziara na kukagua Maendeleo ya Mradi wa Kituo Cha Umahiri katika Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT)leo Julai 13,2023 Jijini Dar es Salaam
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Franklin Rwezimula akimsikiliza Mkuu wa Mafunzo ya uhudumu ndani ya Ndege Bi.Neema Lauo akielezea kuhusu mfano wa ndege zinazotumika kufundishia wanafunzi marubani (Mockup ) wakati alipofanya ziara na kukagua Maendeleo ya Mradi wa Kituo Cha Umahiri katika Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT)leo Julai 13,2023 Jijini Dar es Salaam 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt.Franklin Rwezimula akiongozana na Mkuu wa Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) Prof. Zacharia Mganilwa kukagua Maendeleo ya Mradi wa Kituo Cha Umahiri katika Chuo Cha Taifa Cha Usafirishaji (NIT) leo Julai 13,2023 Jijini Dar es Salaam

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages