Breaking

Monday, 24 July 2023

MRADI WA KILIMO CHA VANILLA WAZINDULIWA DODOMA

Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mnkondya akielezea kuhusu kilimo cha Vanilla kwenye Mradi wa Kilimo cha Vanilla Mkoani Dodoma ‘Vanilla Village Dodoma’.

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog

Kampuni ya Vanilla International Limited imezindua Mradi wa Kilimo cha Vanilla Mkoani Dodoma ‘Vanilla Village Dodoma’ katika kitongoji cha Zamahero Kijiji cha Mayamaya kata ya Zanka wilaya ya Bahi.

Uzinduzi huo ulioambatana na utoaji elimu kwa wananchi wa Dodoma kuhusu kilimo cha Vanilla umefanyika Julai 22,2023 katika Shamba kitalu (Green House) kubwa la Kilimo cha Vanilla kwa njia za kisasa.

Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mnkondya amesema shamba kitalu hilo Mkoani Dodoma ambalo lipo Kilomita 40 kutoka katikati ya Jiji la Dodoma barabara ya Arusha/Barabara ya Kondoa lina ukubwa wa hekta 125.

Amesema zaidi ya Shilingi Bilioni 30 zitawekezwa kwenye kilimo cha Vanila katika mradi huo mkubwa wa miaka mitatu lengo likiwa ni kukuza biashara ya zao hilo na kuzalisha fursa za ajira huku akieleza kuwa uwekezaji huo unakuja baada ya mafanikio makubwa yaliyopatikana katika kilimo cha Vanilla visiwani Zanzibar.

Mnkondya amesema fedha zinazoingizwa katika uwekezaji huo, zitatumika kwenye ujenzi wa nyumba vitalu ili kupata joto na unyevunyevu unahitajika kwa ajili ya ustawishaji wa zao hilo na kwamba nyumba vitalu hivyo pia vitawekewa mfumo wa umwagiliaji maarufu mvuabunduki inayotengeneza umande unaohitajika katika kilimo cha vanilla na kiasi kingine cha fedha kitajenga maabara maalumu ya uchakataji wa zao hilo na ununuzi wa mbegu.

“Hapa Zamahero patakuwa makao makuu ya kilimo cha Vanilla duniani ikiwa mashamba mengine mengine ya Kampuni yetu yapo Zanzibar, Arusha na Kanda ya Ziwa. Dodoma litakuwa shamba kubwa zaidi lenye ukubwa wa hekta 125 ambalo tunafanya uwekezaji wa Shilingi bilioni 30 ndani ya miaka mitatu utakamilika”,ameeleza.

“Kupitia shamba hili tunategemea kuvuna tani 70 za Vanilla kila mwaka na hivyo kuweza kumudu soko la Dubai na Saudi Arabia ambao wanahitaji tani 70 kila mwaka. Bei ya Vanilla kwa Dubai na Saudi Arabia inazidi Dola 600 kwa kilo moja ambayo ni zaidi ya shilingi Milioni 1.3 za Tanzania”,amesema Mnkondya.

KWANINI ZAMAHERO DODOMA?

Akielezea kilichosababisha Kampuni ya Vanilla International Ltd kuanzisha shamba kubwa la kilimo cha kisasa cha Vanilla eneo la Zamahero Mkoani Dodoma, Mnkondya amesema ni kwa eneo hilo lina joto la wastani na baridi ya wastani inayoshawishi na kutengeneza mazingira wezeshi ya kilimo cha Vanilla na kwamba kuna upatikanaji wa umeme kwa sababu Vanilla inatakiwa ichakatwe baada ya kuvunwa.

“Sababu nyingine ni eneo hili linafikika kwa urahisi, hapa kuna upatikanaji wa maji mengi. Katika eneo hili kuna maji ambayo hayana tindikali wala nyongo hivyo kufanya Vanilla isiwe inachubuka na kuoza. Eneo hili ni salama kwa sababu vanilla inahitaji usalama, eneo hili limezungukwa na viongozi akiwemo Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango”,amesema.

“Dodoma eneo hili la Zamahero limezungukwa na wafugaji wengi wa ng’ombe na mbuzi hivyo kufanya upatikanaji wa mbolea/mboji/samadi kuwa rahisi zaidi kwa ajili ya ustawi wa zao. Lakini pia ardhi ya hapa ni bikra bado ina mboji nyingi na rutuba nyingi. Zao hilo lina hitaji wafanyakazi wengi na kutokana na kwamba Dodoma kuna wafanyakazi wengi ndiyo maana tumechagua hapa. Zaidi ya watu 1,350 wataajiriwa”,ameongeza Mnkondya.

Mnkondya ametumia fursa hiyo kuwakaribisha wawekezaji kuwekeza katika eneo hilo kwani ili kuwa uhakika wa bei nzuri lazima mashamba yawe sehemu moja ambapo wakulima wanaweza kutengeneza sauti ya pamoja na kuamua bei.

“Nawaita wawekezaji kuja kuwekeza kwa njia ya block Farming (Mashamba Shufaa/mashamba jumuishi). Mwekezaji badala ya kuwekeza kwenye shamba atapata changamoto ya kupata wataalamu kwa sababu zao linahitaji utaalamu, atapata changamoto ya soko, kwa sababu soko linahitaji mazingira maalumu na uangalizi wa mnunuzi kwenye zao kuepuka wakulima kukosa uaminifu ikiwemo kuweka mchanga, kemikali na madawa mbalimbali kama ilivyo kwa mazao mengine ya biashara nchini”,ameeleza.
Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mnkondya akielezea kuhusu kilimo cha Vanilla kwenye Mradi wa Kilimo cha Vanilla Mkoani Dodoma ‘Vanilla Village Dodoma’ katika kitongoji cha Zamahero Kijiji cha Mayamaya kata ya Zanka wilaya ya Bahi.

Katika hatua nyingine Mnkondya amesema amepata mwaliko wa Kimasoko katika visiwa vya Mauritius Tarehe 5/08/2023 ambapo wenyeji wake huko Mauritius ni wanunuzi wakubwa wa vanilla Duniani. 

Kampuni ya Vanilla International Ltd inajihusisha na kilimo biashara cha Vanilla, masoko ya Vanilla ambazo zimetunzwa chini ya uangalizi wao, utoaji wa elimu na hamasa ya kilimo cha Vanilla, inasafirisha Vanilla nje ya nchi hasa Saudi Arabia na Dubai (Dubai wana kampuni ya nunuzi ya Vanilla – Vanilla Village International trading) ambayo ipo Ajman Free Zone Dubai. Masoko mengine ya Vanilla yapo Ujerumani na Marekani.

Unaweza kujifunza kuhusu Kilimo cha Vanilla kupitia Kampuni ya Vanilla International Ltd kwa kupiga simu namba 0624300200 na 0769300200. Namba hizi zinatumika kwa ajili ya kufundishia wananchi bure kuhusu Kilimo cha Vanilla.

ANGALIA PICHA HAPA CHINI
Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mnkondya akielezea kuhusu kilimo cha Vanilla kwenye Mradi wa Kilimo cha Vanilla Mkoani Dodoma ‘Vanilla Village Dodoma’ katika kitongoji cha Zamahero Kijiji cha Mayamaya kata ya Zanka wilaya ya Bahi leo Jumatatu Julai 24,2023. Picha na Kadama Malunde -Malunde 1 blog
Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mnkondya akielezea kuhusu kilimo cha Vanilla kwenye Mradi wa Kilimo cha Vanilla Mkoani Dodoma ‘Vanilla Village Dodoma’ katika kitongoji cha Zamahero Kijiji cha Mayamaya kata ya Zanka wilaya ya Bahi.
Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mnkondya akielezea kuhusu kilimo cha Vanilla kwenye Mradi wa Kilimo cha Vanilla Mkoani Dodoma ‘Vanilla Village Dodoma’ katika kitongoji cha Zamahero Kijiji cha Mayamaya kata ya Zanka wilaya ya Bahi.
Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mnkondya akielezea kuhusu kilimo cha Vanilla kwenye Mradi wa Kilimo cha Vanilla Mkoani Dodoma ‘Vanilla Village Dodoma’ katika kitongoji cha Zamahero Kijiji cha Mayamaya kata ya Zanka wilaya ya Bahi.
Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mnkondya akionesha Vanilla iliyoanza kulimwa kwenye Shamba kitalu ‘Vanilla Village Dodoma’ katika kitongoji cha Zamahero Kijiji cha Mayamaya kata ya Zanka wilaya ya Bahi.
Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mnkondya akizungumza kwenye Shamba kitalu ‘Vanilla Village Dodoma’ katika kitongoji cha Zamahero Kijiji cha Mayamaya kata ya Zanka wilaya ya Bahi.
Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mnkondya akiangalia Shamba kitalu ‘Vanilla Village Dodoma’ katika kitongoji cha Zamahero Kijiji cha Mayamaya kata ya Zanka wilaya ya Bahi.
Zoezi la kutengeneza vitalu kwa ajili ya kilimo cha Vanilla katika kitongoji cha Zamahero Kijiji cha Mayamaya kata ya Zanka wilaya ya Bahi  Mkoani Dodoma likiendelea
Sehemu ya shamba kubwa kwa ajili ya kilimo cha Vanilla likiendelea kutengenezwa katika kitongoji cha Zamahero Kijiji cha Mayamaya kata ya Zanka wilaya ya Bahi mkoani Dodoma
Mkurugenzi Mwanzilishi wa Makampuni ya Vanilla International Limited, Simon Mnkondya akitoa elimu kwa wananchi wa Dodoma kuhusu kilimo cha Vanilla 

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages