Breaking

Sunday, 2 July 2023

MANUFAA 12 AMBAYO TANZANIA ITAYAPATA KUTOKANA NA UWEKEZAJI WA DP WORLD KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM

 


Zifuatazo ni faida 12 kubwa ambazo Tanzania inatarajia kuzipata kutoka na uwekezaji wa kampuni ya DP World kwenye bandari ya Dar es Salaam:

1. Kupunguza muda wa meli kukaa nangani kutoka siku 5 kwa sasa mpaka masaa 24 tu.

2. Kuongeza idadi ya meli zitakazokuja Bandari ya Dar es Salaam kutoka meli 1,569 zilizohudumiwa mwaka 2021/22 hadi kufikia takriban meli 2,950 ifikapo mwaka 2032/33;

3. Kupunguza muda wa ushushaji wa makontena kutoka wastani wa siku 4.5 mpaka siku 2

4. Kupunguza muda wa uondoshaji mizigo kutoka masaa 12 mpaka saa 1 tu kutokana na uboreshaji wa mifumo yạ TEHAMA;

5. Kupunguza gharama ya usafirishaji wa shehena kutoka nchi za nje kwenda nchi za jirani, kutoka USD 12,000 mpaka kati ya USD 6,000 na USD 7,000 kwa kasha

6. Kuongezeka kwa shehena inayohudumiwa kutoka tani milioni 18.41 kwa mwaka 2021/22 hadi kufikia tani milioni 47.57 mwaka 2032/33

7. Kuongezeka kwa mapato ya serikali yatokanayo na kodi ya forodha inayokusanywa katika shehena inayopitishwa bandarini kutoka Shilingi trilioni 7.76 kwa mwaka 2021/22 hadi Shilingi trilioni 26.70 kwa mwaka 2032/33

8. Kuongezeka kwa ajira zinazotokana na shughuli za bandari kutoka 28,990 kwa mwaka 2021/22 hadi 71,907 ifikapo mwaka 2032/33

9. Maboresho ya magati  ya kuhudumia majahazi na abiria ikiwa ni pamoja na kushawishi uingiaji wa meli kubwa za kitali (cruise ships) zitakazo ongeza idadi ya watalii nchini na kuongeza pato la taifa

10. Mafunzo ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa TPA katika Bandari zote (knowledge and skills transfer)

11. Uanzishaji wa maeneo huru ya kiuchumi na kuchochea ukuaji wa sekta zingine za kiuchumi zikiwemo: sekta ya kilimo, mifugo na uvuvi; utali; viwanda na biashara

12. Kuchagiza ukuaji wa sekta ndogo za usafirishaji kwa njia ya reli (SGR, TAZARA na MGR) na barabara; na kuimarisha mahusiano ya kidiplomasia.

Chanzo: Takwimu kutoka Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages