Katibu Mkuu Wizara ya Nishati Mhandisi Felchesmi Mramba amesisitiza Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST) kuendelea kufanya tafiti zaidi ikiwemo kuongeza uelewa kwa wananchi kuhusu uwepo wa madini mbalimbali nchini
Mhandisi Mramba amebainisha hayo leo Julai 3, 2023 alipotembea banda la Wizara ya Madini, Taasisi za Wizara na Wadau wa Sekta ya Madini katika Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba jijini Dar es Salaam.
Aidha, ameishauri GST kusambaza vitabu vya Madini yapatikanayo Tanzania toleo Jipya 2023 kwa wananchi ili waweze kutumia taarifa hizo ambazo ni muhimu.
Mbali na GST ametembelea washiriki mbalimbali katika Banda la Wizara.