Breaking

Friday, 21 July 2023

KATAMBI AGAWA MAJIKO YA GESI SHINYANGA MJINI

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (wa pili kushoto) akikabidhi majiko ya gesi yaliyotolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi  (aliyevaa shati la kijani) ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kwa mpika/muuza kahawa mjini Shinyanga

Na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini ametoa msaada wa Majiko 665 ya Gesi yenye thamani ya shilingi milioni 30 kwa wajasiriamali wakiwemo wauza kahawa, mama lishe na baba lishe na makundi mbalimbali ya wananchi katika jimbo hilo lenye jumla ya kata 17 ili kutunza mazingira kwa kutumia nishati mbadala na kumtua mama kuni kichwani.

Hafla ya makabidhiano ya Majiko hayo ya gesi iliyoambatana na utoaji elimu kuhusu matumizi ya majiko ya gesi imefanyika leo Ijumaa Julai 21,2023 katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga ambapo mgeni rasmi alikuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkuu huyo wa Mkoa amempongeza Mhe. Katambi kwa jihihada mbalimbali anazofanya katika kuwaletea maendeleo wananchi wa Shinyanga huku akieleza kuwa majiko hayo ni sehemu ya utunzaji mazingira kwa kutumia nishati mbadala ili kuepukana na matumizi ya kuni na mkaa lakini pia kupunguza muda wa kupika.

“Asante sana Mhe. Mbunge kwa kutuletea majiko haya Rafiki kwa mazingira, sasa tutapika kwa wakati mfupi na urembo wetu utaongezeka kwa sababu hatuchafuki. Tunakushukuru kwa kuwajali wananchi kata zote za Jimbo la Shinyanga. Nendeni mkatumie majiko haya ya kisasa na ndoa zitaenda kuimarika”,amesema Mndeme.
“Kati ya wabunge wanaofanya kazi vizuri, Katambi yumo. Katambi ni kijana mchapakazi na msikivu sana, mlifanya maamuzi sahihi kuchagua mbunge huyu. Naomba tumuunge mkono, tusimkatishe tamaa, tumtie moyo na tumuunge mkono kwa kumpa ushirikiano, huyu ni mtoto wetu tusitafute mtoto mwingine”,amesema Mhe. Mndeme.

“Hapa tulipo tunafanya kazi ya utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM, na Mbunge huyu anatekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM kwa vitendo”,ameongeza.

Katika hatua nyingine Mhe. Mndeme amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa fedha nyingi anazoendelea kutoa kwa ajili ya maendeleo katika sekta mbalimbali.

Aidha amewahakikishia wajasiriamali na wafanyabiashara kuwa serikali itaendelea kuwapa ushirikiano huku akiwahakikishia kuwa hakuna mtu atawasumbua kwenye maeneo yao ya biashara.

Katika hatua nyingine amewataka wananchi kuwapuuza baadhi ya watu wanaopotosha kuwa Bandari ya Dar es salaam na nchi imeuzwa akisema serikali ina nia njema ya kufanya uwekezaji kwenye bandari ili kuongeza tija kwa ajili ya maendeleo ya nchi.
Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini 

Kwa upande wake, Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mhe. Patrobas Katambi amesema ataendelea kutoa majiko ya gesi kwa makundi mbalimbali ya wananchi katika jimbo hilo kwani serikali imedhamiria kumtua mama kuni kichwani.

“Kauli mbiu yetu ni Shinyanga yetu, jukumu langu na tunatoa majiko haya ya gesi kwani tumedhamiria kumtua ndoo mama kichwani, tumeweza na sasa tunamtua mama kuni kichwani.Tumeanza na viongozi tumewapa majiko ya gesi lakini pia wamepewa elimu ya matumizi ya majiko ya gesi”,amesema Katambi.

“Nilipiga hodi Kampuni ya Oryx kwa ajili ya mahitaji ya majiko ili kumuunga mkono Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan katika kutunza mazingira. Tunamtua mama kuni kichwani, leo ni awamu ya kwanza, tutakuja awamu ya pili kugawa majiko ya gesi kwa makundi mbalimbali ya wananchi”,amesema Katambi.

Katika hatua nyingine amesema serikali imeendelea kuleta maendeleo mbalimbali katika sekta ya barabara, maji, elimu, afya na sekta zingine na kwamba inaendelea kutoa fedha kwa ajili ya maendeleo.

Kuhusu Uwekezaji katika Bandari, Mhe. Katambi amesema jambo hilo lina ugumu katika kulielewa kwa sababu kuna baadhi ya wanasheria hawajalielewa vizuri licha ya kwamba ni wanasheria kwa sababu ni jambo la kitaalamu zaidi.

"Watanzania wasiburuzwe kwenye jambo, watanzania watoe maoni kwa ajili ya maslahi ya nchi. Kinachofanyika ni uboreshaji kwenye Bandari, ifike mahali tuwaamini viongozi wetu, kama hakuna maslahi ya nchi hatuwezi kukubaliana",amesema Katambi.

Nao baadhi ya wananchi walionufaika na msaada huo wamemshukuru Mhe. Katambi kwa kuwapatia majiko hayo ya gesi.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati akikabidhi majiko ya gesi yaliyotolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kwa wajasiriamali na viongozi wa makundi mbalimbali katika Jimbo la Shinyanga Mjini leo Ijumaa Julai 21,2023 katika ukumbi wa CCM Mkoa wa Shinyanga. Picha na Kadama Malunde - Malunde 1 blog
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akizungumza wakati akikabidhi majiko ya gesi yaliyotolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kwa wajasiriamali na viongozi wa makundi mbalimbali katika Jimbo la Shinyanga Mjini

Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini akizungumza wakati wa kukabidhi majiko ya gesi kwa wajasiriamali na viongozi wa makundi mbalimbali katika Jimbo la Shinyanga Mjini

Muonekano wa sehemu ya majiko ya gesi yaliyotolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kwa wajasiriamali na viongozi wa makundi mbalimbali katika Jimbo la Shinyanga Mjini

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (wa tatu kushoto) akikabidhi majiko ya gesi yaliyotolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi  (aliyevaa shati la kijani) ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kwa wajasiriamali na viongozi wa makundi mbalimbali katika Jimbo la Shinyanga Mjini
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme (wa pili kushoto) akikabidhi majiko ya gesi yaliyotolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi  (aliyevaa shati la kijani) ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kwa wajasiriamali na viongozi wa makundi mbalimbali katika Jimbo la Shinyanga Mjini

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Kampuni ya Oryx, Peter Ndomba akizungumza wakati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mhe. Christina Mndeme akikabidhi majiko ya gesi yaliyotolewa na Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Patrobas Katambi ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini kwa wajasiriamali na viongozi wa makundi mbalimbali katika Jimbo la Shinyanga Mjini
Maafisa kutoka Kampuni ya Oryx wakitoa elimu ya matumizi ya jiko la gesi
Katibu wa CCM Wilaya ya Shinyanga Mjini Ally Majeshi akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji majiko ya gesi
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Shinyanga Dkt. Christina Mnzava akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji majiko ya gesi
Madiwani wakizungumza wakati wa hafla ya ugawaji majiko ya gesi
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Shinyanga Mhe. Elias Masumbuko akizungumza wakati wa hafla ya ugawaji majiko ya gesi
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages