Breaking

Friday, 14 July 2023

KAMISHENI YA BONDE MTO SONGWE YAJIPANGA UJENZI WA BWAWA LA MAJI

Waziri wa Maji Tanzania na Mwenyekiti Mwenza wa Baraza la Mawaziri Bonde la Mto Songwe Mhe. Jumaa Aweso ameongoza Mkutano wa pili wa Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe.

Waziri Aweso ambaye ni Mwenyekiti Mwenza na Mwenyeji ameshirikiana na Mwenyekiti mwenza wa Kamisheni kutoka Malawi Waziri wa Maji Mhe. Abida Sidik Mia ambapo kwa pamoja wameongoza mkutano huu wa siku moja ukijadili maendeleo ya pamoja ya ushirikiano katika kamisheni ya Bonde la Mto Songwe , kujadili na kupitisha makadirio ya Bajeti, kujadili maendeleo na undeshaji wa Kamisheni, na na dhima kuu na lengo maalum la mkutano huu ambalo ni maandalizi ya ujenzi wa bwawa la kuhifadhi Maji, Mto Songwe kwaajili ya kuzuia mafuriko, matumizi ya Binadamu, shughuli za kilimo, pamoja na kuzalisha Nishati ya Umeme ikiwa wajumbe wamekubaliana mchakato wa kutafuta fedha na hatua za ujenzi ziendelee.

Mkutano huu umewajumuisha Wajumbe wa Baraza la Mawaziri wa Kamisheni ya Bonde la Mto Songwe kutoka Malawi na Tanzania wanaotokana na Sekta 5 kwa nchi zote mbili ikiwa ni pamoja na Maji, Nishati, Ardhi, TAMISEMI, na Kilimo. Mkutano umeudhuliwa na Waziri wa Ardhi na Makazi Mhe Angelina Mabula, N/Waziri wa TAMISEMI Mhe Deogratius Ndejembi, N/Waziri wa Kilimo Mhe Anthony Mavunde na N/Waziri wa Nishati Mhe Stephen Byabato.
Kutoka Malawi ni Mhe. Matola Ibrahim, Mhe. Oweni Chumanika, na Mhe. Deus Gumba.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages