NA MWANDISHI WETU
Wanafunzi wa Shule ya Awali ya Little Step iliyopo Mikocheni Jijini Dar es Salaam wametembelea Banda la Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika Viwanja vya Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara Dar es Salaam vijulikanavyo kama Sabasaba mapema Leo tarehe 5 Julai, 2023
Shule hiyo imetembelea Banda Hilo kwa lengo la kupata elimu ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto.
Akizungumza mara baada ya kuwapokea Wanafunzi hao, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano kwa Umma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi (SACF) Puyo Nzalayaimisi amesema mara nyingi wamekuwa wakitoa elimu hiyo katika maeneo mbalimbali ikiwemo katika mikusanyiko ya watu, sokoni, stendi za mabasi pamoja na shule.
Pamoja na utoaji wa elimu katika makundi mbalimbali bado kuna changamoto ya utoaji wa taarifa wakati kwa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati wa dharura.
Aidha imetulazimu kutumia mbinu mbalimbali za kufikisha elimu kwa kubadili mfumo wa utoaji elimu hiyo na kuwa ya vitendo zaidi.
Kati ya mbinu hizo ni pamoja na hii ya Leo ambayo mmeona Wanafunzi hawa wameweza kupata elimu kwa kuchora, kupaka rangi magari ya kuzimia moto na namba ya dharura ya Jeshi pamoja na kujua matumizi mbalimbali ya vifaa vya kuzimamoto vya awali.
Naamini siku hii ya leo tumeweza kutengeneza MABALOZI wa kudumu wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kupitia elimu waliyoipata Wanafunzi hawa wa Little Steps.
"Tuwe na utamaduni wakuwapatia elimu ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga watoto wetu kwani ni taifa la kesho" amesema SACF Puyo.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu wa Shule ya Little Steps Bi. Grace Mushi amesema waliona ni muhimu Watoto kupata elimu ya kinga na tahadhari ya majanga mbalimbali kwa kuwa kwa namna moja au nyingine watoto wamekua chanzo cha moto mingi bila kujijua kwa kuchezea vitu hatarishi kama vibiriti na mishumaa.
Walimu na wanafunzi hao wamefurahia mafunzo na elimu waliyoipa na kuahidi kuwa mabalozi wazuri katika jamii na wataendelea kujifunza na kufuatilia elimu inayotelewa na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.