Breaking

Tuesday, 4 July 2023

JESHI LA ZIMAMOTO NA UOKOAJI LASHIRIKI MAONESHO SABASABA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

JESHI la Zimamamoto na Uokoaji linashiriki Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba Jijini Dar es Salaam, ambapo limewakaribisha wadau na wananchi kwa ujumla kutembelea banda lao lililopo mkabara na banda la Jeshi la Polisi kuona na kufahamu majukumu makubwa yanayofanywa na jeshi hilo.

Akizungumza leo Julai 4,2023 katika Maonesho hayo, Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Ilala Jijini Dar es Salaam, Christina Sanga amesema wanatoa elimu kuhusu matumizi sahihi ya vifaa vya uokoaji, huduma ya kusoma ramani pamoja na huduma zingine ambazo zinahusiana na kuzima moto na kuokoa maisha ya watu na mali zao.

Nae Mkuu wa Kitengo cha Elimu kwa Umma, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Puyo Nzalayaimisi amesema Maonesho hayo yameelekezwa zaidi kwa wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, hivyo basi watawaelimisha ni namna gani ambavyo wao Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wamejiweka kimkakati katika kukabiliana na majanga viwandani.

Pamoja na hayo amesema kupitia maonesho hayo mtu anaweza kuleta ramani yake na ataweza kupata elimu ya namna ya kujikinga na majanga kwasababu kuna vifaa watamuonesha na kumpa elimu namna ya kuvutumia.

Pamoja na hayo amesema wanatarajia kuzindua program maalumu ya kufundiahia watoto namna ya kujikinga na majanga ya moto.

"Tumekuwa tukizunguka kwenye mashule na sehemu mbalimbali, tumebuni namna tofauti ya kukabiliana na majanga hasa kuwafundisha watoto, tunavitabu vinavyoelekeza vifaa, aina ya moto na namna ya kukabiliana na haya majanga". Amesema Puyo

Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Ilala Jijini Dar es Salaam, Christina Sanga akitembelea baadhi ya mabanda ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam,


Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Ilala Jijini Dar es Salaam, Christina Sanga akitembelea baadhi ya mabanda ya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji katika Maonesho ya 47 ya Biashara ya Kimataifa Sabasaba yanayoendelea Jijini Dar es Salaam,



(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages