Polisi wanachunguza kisa ambapo mwanaume mmoja alijitoa uhai baada ya mkewe kuripotiwa kukataa kupika kuku.
Kisa hicho cha kushangaza kimeripotiwa katika kaunti ya Migori eneo la Uriri nchini Kenya ambapo sasa majirani wako kinywa wazi kwa mshangao.
Afisa Msaidizi wa Nyaobe, John Atonya, alisema mwanaume huyo mwenye umri wa miaka 45 alijifungia ndani ya nyumba yao kabla ya kujiwasha moto.
"Mwanaume huyo, ambaye anajulikana kwa jina la John Rugala, alijifungia ndani ya nyumba kabla ya kuichoma moto. Inadaiwa kuwa mkewe alikataa kupika kuku kwa ajili yake," Atonya alisema.
Ripoti za awali zinaonyesha kuwa mkewe hakukubaliana na wazo hilo kwani kuku huyo ambaye hawezi kuruka alikuwa mali ya binti yao.
"Aliupinga baada ya mkewe kumtaka apate kibali kutoka kwa binti yake ambaye ndiye mwenye kuku hao," aliongeza afisa huyo.
Ripoti ya Citizen Digital ilionyesha kuwa marehemu anasemekana kumfukuza mkewe kabla ya kuchukua maisha yake.
Wananchi walikimbilia eneo la tukio kujaribu kuzima moto lakini juhudi zao hazikuzaa matunda.
Atonya alisema mwili wa marehemu umehamishiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti cha Hospitali ya Migori Level Four wakati uchunguzi wa polisi ukiendelea.
Polisi sasa wanafuatilia kwa karibu kujua iwapo chanzo cha mzozo baina ya wawili hao ilikuwa tu ni kuku au kulikuwa na mengine.
Chanzo: TUKO News