Breaking

Tuesday, 4 July 2023

GGML KUTUMIA SHILINGI BILIONI 6 UJENZI UWANJA WA MPIRA GEITA






#Kukamilika kwake kuhamasisha shughuli za Michezo

# Timu mbalimbali zikiwemo Simba, Yanga, Azam FC, na nyingine kuutumia uwanja huo

Imeezwa kuwa, Mradi wa Ujenzi wa Uwanja wa Mpira wa Miguu unaoendelea katika eneo la Magogo Mkoani Geita unakadiriwa kugharimu kiasi cha shilingi bilioni 6.




Hayo yameelezwa leo Julai 4, 2023 na Afisa Uhusiano wa Kampuni ya Geita Gold Mining Ltd Doreen Dennis katika banda la kampuni hiyo katika Maonesho ya Kimataifa ya 47 ya Sabasaba yanayoendelea jijini Dar es Salaam.




" Uwanja wetu wa Magogo utakapo kamilika unakadiriwa kuchukua zaidi wa mashabiki elfu 20 kwa wakati mmoja ili kutazama mechi mbalimbali zitakazochezwa katika uwanja huo," amesema Doreen.




Ameongeza kuwa, uwanja wa Magogo utakuwa kivutio kikubwa kwa wananchi wa mkoa wa Geita na Kanda ya ziwa kwa ujumla. Amesema mbali ya michezo,unatarajiwa kukuza uchumi kwa wakazi wa Geita na kuhamasisha Michezo.




Doreen ameongeza kwamba uwanja huo unatarajiwa kukamilika mwaka huu 2023 na kampuni ya GGML inatarajia kuukabidhi kwa halmashauri ya Mji wa Geita huku pia ukitumika kama uwanja wa nyumbani wa timu ya Mpira ya Geita Gold FC ambayo inacheza Ligi Kuu Tanzania Bara.




Kampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) ndiyo mdhamini mkuu wa timu hiyo.















Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages