Breaking

Wednesday, 19 July 2023

DKT. MSONDE AINYOSHEA KIDOLE KILOMBERO UCHELEWESHAJI WA MIRADI YA ELIMU



OR TAMISEMI

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI (Elimu), Dkt. Charles Msonde amezinyoshea kidole halmashauri za Mji wa Ifakara na Halmashauri ya Wilaya Mlimba wilayani Kilombero kwa ucheleweshaji wa ujenzi wa miundombinu ya elimu ya msingi na Sekondari.

Dkt. Msonde ameonesha hali ya kutoridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya elimu ambayo inaendelea kutekelezwa katika wilaya ya Kilombero mkoani Morogoro tarehe 18 Julai 2023.

“Halmashauri ya Mji wa Ifakara na Mlimba bado mpo nyuma sana katika utekelezaji wa miundombinu ya elimu msingi kupitia mradi wa BOOST na ujenzi wa miundombinu kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha tano” amesema Dkt. Msonde.

Dkt. Msonde amesema maeneo mengine yanatekeleza miradi hiyo wameshakamilisha na wengine waliochelewa wapo katika hatua za kumalizia kwa kupaka rangi lakini katika halmashauri hizo bado wapo nyuma sana.

Aidha, amesema katika ujenzi wa miundombinu ya upanuzi wa shule za Sekondari kwa ajili wanafunzi wa kidato cha tano bado wako nyuma ambapo miundombinu yote inapaswa kukamilika ifikapo tarehe 30 Julai 2023 ili iweze kupokeaa wanafunzi hao watakaoanza masomo tarehe 13 Agosti 2023.

Kutokana na hali hiyo, Dkt. Msonde amemuagiza Mkuu wa Wilaya Kilombero kuhakikisha anasimamia maeno yote ambayo yapo nyuma katika ujenzi kufungwa taa zenye mwanga ili kazi ya unjezi ifanyika usiku na mchana bila kuathiri ubora na viwango.

Kadhalika, ameagiza maeno yote ya ujenzi kuongezwa nguvu kazi ya Mafundi ili kufanya kazi kubwa kwa muda mfupi ikiwa ni pamoja na kufanya kazi zinazoenda sambamba kwa wakati mmoja.

Dkt. Msonde amewataka Wakurugenzi na Wahandisi wa halmashauri hizo kwa kushirikiana na Maafisa elimu kuweka uangalizi wa karibu kwa kusimamia na kukagua kila hatua inayoendelea katika ujenzi wa miundombinu hiyo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages