Breaking

Monday, 3 July 2023

DIT YAJA NA TEKNOLOJIA YA NGOZI YA SAMAKI KWENYE MAONESHO SABASABA

TAASISI ya Teknolojia Dar es Saam (DIT) kupitia kampuni tanzu imekuja na teknolojia ya ngozi ya Samaki aina ya Sangara ambao wanapatikana katika ziwa Victoria.

Akizungumza leo Julai 2,2023 katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, jijini Dar es Salaam, Mwalimu wa DIT Kampas ya Mwanza, Bw.William Lohay amesema ngozi hizo ni kama mabaki ya kutoka kwenye viwanda ambavyo vinachakata minofu ya samaki.

"Tumeona tuweze kutumia bidhaa hii ya ngozi ya samaki na kuzichakata ili iweze kutumika kuandaa bidhaa zingine mbalimbali ambazo zinatumika kupitia ngozi". Amesema Bw. Lohay.

Aidha Bw.Lohay amesema baada ya kupima uwezo wa ngozi hiyo wameona inafaa kutengenezea bodhaa mbalimbali kama vile mikanda, mikoba na muda mwingine unaweza kuitumia kwenye viatu kwa kuweka kipande cha ngozi ya samaki na kuweza kupendezesha bidhaa yako.

"Ngozi ya samaki iko imara na inanguvu sawasawa na ngozi zingine. Na katika upande wa uimara kimsingi ziko imara hata kuzizidi ngozi za mbuzi kwani zinakatibiana na uimara wa ngozi za ng'ombe". Amesema

Pamoja na hayo amesema kuwa sekta ya viwanda vya ngozi wanaweza kutumia ngozi ya samaki kama moja ya malighafi ya kutengenezea ngozi ambayo itatumika kwaajili ya kutengenezea bidhaa za ngozi.

Ameeleza kuwa moja ya faida ya ngozi ya samaki, inapunguza uchafuzi wa mazingira kwa maana ngozi ya samaki hazina manyoya tofauti na wanyama wengine.

"Wakati wa kuichakata ngozi ya samaki ni rahisi, yake magamba yanatoka na unaweza kuyakusanya na ukatengeneza bidhaa nyingine ambayo unaweza kubuni, mfano gundi". Ameeleza.
Mwalimu wa DIT Kampas ya Mwanza, Bw.William Lohay akionesha ngozi ya samaki pamoja na bidhaa za ngozi hiyo leo Julai 3 katika Maonesho ya 47 ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam (TanTrade), Tanzania, Jijini Dar es SalaamBaadhi ya bidhaa za ngozi ya Samaki


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages