Na Nelson Shoo - Zanzibar
Timu ya mpira wa Pete ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es salaam (DAWASA) imeinyuka mabao 86 kwa mabao 9 timu ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Musoma (MUWASA) katika michuano ya Maji Cup msimu wa tatu yanayoendelea visiwani Zanzibar.
Mchezo huo umechezwa katika viwanja vya Gymkhana ikiwa ni mchezo wao wa pili katika mashindano hayo ambapo kwa mchezo wa kwanza DAWASA ilikula kichapo cha goli 29 kwa 56 dhidi ya timu ya MBEYA WSSA.
Kocha wa timu hiyo Ndugu Abdallah Juma akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo amesema lengo la timu ni kuchukua ubingwa wa michuano hiyo japo hawakuanza vizuri lakini leo wachezaji wameonyesha kiwango cha kuridhisha.
"Tunashukuru uongozi mzima wa DAWASA kwa kutupa nafasi hii, tumekuja kupambana na tunauhakika tutaibuka washindi wa michuano hii kwani wachezaji wamejiandaa vyema." amesema Kocha Abdallah