Breaking

Saturday, 22 July 2023

CHONGOLO AWASILI KANDA YA KASKAZINI, KUFANYA MKUTANO MKUBWA WA HADHARA JIJINI ARUSHA LEO .

KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Ndugu Daniel Chongolo amewasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) mapema leo asubuhi, tayari kuelekea jijini Arusha kufanya mkutano mkubwa wa hadhara utakaofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Jumamosi ya Julai 22,2023.

Akiwa ameambatana na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Ndugu Stephen Wassira na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mipango na Uwekezaji, Ndugu Kitila Mkumbo, Katibu Mkuu Chongolo baada ya kuwasili uwanja wa ndege, amelakiwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wa mikoa ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara.

Katika mkutano huo wa leo, pamoja na mambo mengine Katibu Mkuu Chongolo ataelezea hatua kwa hatua usahihi wa makubaliano ya uwekezaji kwa ajili ya kuboresha uendeshaji na ufanisi wa Bandari ya Dar es Salaam, lengo likiwa kuhakikisha bandari hiyo inatoa huduma kwa viwango vya hali ya juu tofauti, ili kuongeza, tofauti na ilivyo sasa.



Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages