Breaking

Sunday, 2 July 2023

BASI LATEKETEA KWA MOTO NA KUUA WATU 25




Zaidi ya watu 25 wameaga dunia baada ya basi lilikokuwa limebeba kundi la watu waliokuwa kwenye sherehe ya harusi kupata ajali na kuteketea magharibi mwa India.

Kwa mujibu wa ripoti ya CNN ya India, News 18, Naibu Msimamizi wa Polisi huko Buldhana Baburao Mahamuni, maafa hayo yalitokea katika jimbo la Maharashtra mnamo Jumamosi.

Mahamuni anasema kuwa waliopata majeraha katika tukio hilo kwenye barabara kuu ya Samruddhi Mahamarg walipelekwa katika Hospitali ya Wilaya ya Buldhana.

Polisi wanaamini basi lilipata ajali kutokana na mvua saa mbili asubuhi wakati lilikuwa likisafiri kutoka Yavatmal kwenda Pune na tenki lake la dizeli likashika moto.

News 18 ilichapisha tafsiri ya ujumbe wa gavana wa Maharashtra Eknath Shinde ambapo alitoa rambirambi na kutoa fidia kwa ndugu wa marehemu.

"Gavana Eknath Shinde ameelezea huzuni kubwa juu ya ajali mbaya ya basi la kibinafsi kwenye barabara kuu ya Samruddhi karibu na Sindkhedaraja katika wilaya ya Buldhana," ulisema ujumbe huo.

Ulisema Mfuko wa Msaada wa Gavana utatoa takriban dola 6,000 kwa familia za kila mtu aliyeuawa "katika tukio hili lisilofaa."

Via: Tuko news

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages