Breaking

Wednesday, 12 July 2023

AMUUA JIRANI YAKE KWA PANGA AKIMTUHUMU KUMUIBIA SIMU, PESA


Picha haiendani na tukio


Maafisa wa polisi katika kaunti ya Bomet nchini Kenya wanamzuilia mwanamume mmoja kwa kumdunga kwa kisu na kumuua jirani yake kwa tuhuma za kumwibia simu na Ksh 1800 ( 31,000 Tsh).

Polisi wanasema kuwa Amos Cheruiyot mwenye umri wa miaka 25 aliingia kimyakimya usiku katika nyumba ambayo mwendazake alikuwa amepewa makazi na rafiki yake.

Kulingana na Afisa wa eneo la Sugurmega, Richard Byegon, Cheruiyot alimshambulia kwa panga mwendazake aliyekuwa na umri wa miaka 36 hadi akaaga dunia.

Byegon anasema kuwa mtuhumiwa na marehemu walijulikana kuwa marafiki na walikuwa wakisafiri pamoja na kutembeleana na familia zao kabla ya tukio hilo lisilofurahisha.

Polisi walisema kuwa marehemu alifariki kutokana na majeraha makubwa kwenye kichwa, mikono, na miguu wakati alipokuwa akipelekwa hospitali ya Rufaa ya Kaunti ya Longisa ambapo mwili umehifadhiwa tangu wakati huo.

Wananchi walimkamata mtuhumiwa na kumpeleka kituo cha polisi.

Kamanda wa polisi wa kaunti ndogo ya Chepalungu, Phanton Analo, alisema silaha ya mauaji ilipatikana na eneo la tukio limeshughulikiwa.


Via: Tuko News
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages