Waziri wa Nchi,Ofisi ya Waziri Mkuu,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu ,Mhe.Joyce Ndalichako jana tarehe 12/6/203 alihutubia Baraza la kazi Duniani jana makao makuu ya Un,Jijini Geneva nchini Uswisi na kuonyesha juhudi za Nchi zilizofikiwa katika maeneo mbali mbali yakiwemo Sheria za kazi, ajira na jinsi.
Aidha katika hotuba yake ,Mhe. Ndalichako alieleza kuwa Tanzania inavvyo fuata Mikataba ya kimataifa kuhusu masuala ya kazi, ajira,hifadhi ya jamii na ushirikishwaji wa sauti za makundi mbali mbali kutoka kwa waajiri na wafanyakazi.
Tanzania ni moja kati ya nchi zilizofanya vizuri katika sekta ya hifadhi ya jamii kwa kuanzisha sheria inayoruhusu watu walio katika sekta isiyo rasmi kuchangia na kunufaika na mafao ya hifadhi ya jamii. Aidha, imekua miongoni mwa nchi za mfano katika kutekeleza programu ya mafunzo ya uanagenzi.