Breaking

Thursday, 8 June 2023

WAZIRI MKUU MGENI RASMI KONGAMANO LA KUJENGA UELEWA KUHUSU ATHARI ZITOKANAZO NA SAUTI KWENYE NYUMBA ZA IBADA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

BARAZA la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) kwa kushirikiana na Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) wameandaa kongamano la Kitaifa la kujenga uelewa kuhusu athari zitokanazo na sauti zilizozidi viwango katika nyumba za ibada litakalofanyikaJuni 12,2023 Jijini Dar es Salaam.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Juni 8,2023  Mwenyekiti Taifa -Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT), Sheikh Dkt.Alhad Issa Salum amesema katika Kongamano hilo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Kassim Majaliwa hivyo amewataka viongozi wa wote wa dini na madhehebu yote kuhudhuria ili kuweza kupata fursa ya kuelewa na uelewa wa hizo athari zitokanazo na sauti zilizozidi viwango.

Amesema kongamano  hilo litawajengea uelewa zaidi katika lile linalokusudiwa na kupelekea waumini na wananchi wote kuishi kwa amani na utulivu.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mkuu NEMC, Dkt.Samuel Gwamaka amesema kwa kipindi  hiki wamewalenga hasa viongozi wa dini pamoja na viongozi wa kimila hivyo amewataka wafike ili kuwapatia elimu itakayowaandaa kuwa mabalozi wazuri wa mazingira kwa watu wanaowaongoza.

"Tunaamini kwamba kwa kutoa elimu hii inayohusiana na suala la mazingira katika maeneo mbalimbali yanayogusa jamii hasa kwenye masuala ya kiafya viongozi hawa watakuwa mabalozi wazuri kufikisha elimu hiyo  kwa wale ambao wanawalea katika nidhamu". Amesema Dkt.Gwamaka.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages