MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) limefanikiwa kusajili watoa huduma binafsi na Utoaji vibali vya uendeshaji 107 wa magari yanayotoa huduma za Usafi wa Mazingira Dar es Salaam ambao wamejitokeza katika kioindi ambacho kiliwekwa.
Madhumuni ya zoezi hilo ni kupata takwimu zao ili DAWASA iwafahamu ni watu gani ambao wanafanya nao kazi ili waweze kutoa huduma pamoja nao katika kuhakikisha usafi wa mazingira unaboreshwa kikamilifu kwenye Mkoa wa Dar es Salaam.
Zoezi hilo linafanyika Mwezi Juni 23,2023 na kufikia tamati 30,2023 katika eneo la mabwawa ya vingunguti Jijini Dar es Salaam ambapo watoa huduma walifika eneo hilo na kuweza kusajiliwa bila malipo.