Breaking

Friday, 30 June 2023

UKOSEFU WA HUDUMA YA MAJI KWA WAKAZI WA WANAOHUDUMIWA NA MTAMBO WA RUVU JUU




Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) inawatangazia wateja na Wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji Ruvu juu kuwa, kutakuwa na ukosefu wa huduma ya maji kwa muda wa saa 24 kwa siku ya Jumamosi 1/07/2023 kuanzia saa 12 jioni hadi Jumapili 02/07/2023 saa 12 jioni.

Sababu: Kuruhusu matengenezo za pampu za kusukuma majisafi kutoka mtamboni kwenda kwa wananchi.

Maeneo yatakayoathirika ni;
Ruvu darajani, Ruvu JKT, Mlandizi, Mbwawa, Visiga, Mile 35, Misugusugu, Kongowe, Soga, Miembe saba, Kwa Mfipa, Mwendapole, Tanita, Kwa Mathias, Kwa Mbonde, Pichandege, Lulanzi, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Magari Saba, Mbezi inn, Mbezi, Kimara,Tabata, Kinyerezi, Kisukuru, Msigani, Maramba mawili, Tabata, Kimara B, Kimara Korogwe, Bucha, Baruti, pamoja na Ubungo

Tafadhali kumbuka kuhifadhi maji ili kuwa na hifadhi ya kutosha kipindi chote cha matengenezo.

Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kupitia kituo cha huduma kwa wateja 0800110064 (bure) au
0735 202 121(WhatsApp tu)

Tovuti: www.dawasa.go.tz

Mitandao ya kijamii.

Facebook: https://www.facebook.com/pg/Dawasaofficial/posts/

Instagram: https://instagram.com/dawasatz?utm_medium=copy_link

Twitter: https://twitter.com/dawasatz?s=08

YouTube: https://youtube.com/channel/UCCVyHKIvUwDFG1tUyWhd7fQ

Imetolewa na
Kitengo cha Mawasiliano
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages