Breaking

Monday, 19 June 2023

RAIS SAMIA MGENI RASMI MAADHIMISHO SIKU KIMATAIFA YA KUPIGA VITA DAWA ZA KULEVYA



******************

RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk.Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika maadhimisho Siku ya Kimataifa ya kupiga vita dawa za kulevya ambayo kitaifa yatafanyika Juni 25 mwaka huu wenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha.

Akizungumza leo Juni 19,2023 jijini Dar es Salaam Kamishina Jenerali wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya Aretas Lyimo amesema Mamlaka hiyo inawataarifu watu wote kuwa, Juni 26 Juni kila mwaka, Tanzania huungana na mataifa mengine kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Kupiga Vita Dawa za Kulevya Duniani.

Lengo la siku hiyo ni kuongeza uelewa wa jamii na kuhamasisha Umma kushiriki katika mapambano dhidi ya matumizi na biashara ya dawa za kulevya huku akifafanua maadhimisho haya kwa mwaka huu kitaifa, yatafanyika kuanzia Juni 23 Juni, hadi Juni 25 2023 jijini Arusha.

“Maadhimisho haya yataambatana na maonesho ya shughuli mbalimbali za udhibiti zinazofanywa na Mamlaka pamoja na wadau wake katika udhibiti wa dawa za kulevya na utoaji elimu kuhusu tatizo la dawa za kulevya.Mgeni rasmi siku ya kilele tarehe 25 Juni, 2023 ni Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan.

“Kauli mbiu ya maadhimisho haya ni “Tuzingatie Utu na Kuboresha Huduma za Kinga na Tiba”. Wananchi wote hususani wakazi wa Arusha na mikoa ya jirani mnakaribishwa kushiriki katika maadhimisho hayo,”amesema Kamishina Jenerali Lyimo.
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages