Na Said Mwishehe,
HAPA juzi kati mtu wangu mwenzio nilibahatika kutembelea baadhi ya hifadhi za misitu ya asili pamoja na miti ya kupanda katika mikoa ya Kagera, Geita na Mkoa wa Mara
Ndio kwa Kagera nilikwenda Shamba la Miti Rubare ambapo mbali ya msitu mkubwa wa miti nikapata fursa ya kuona na utalii Ikolojia uliomo ndani ya shamba hilo, ni kuzuri balaa, meza mate kwanza halafu tutaendelea, nitakueleza vizuri tu, subiria mwana.
Lakini baada ya kwenda Rubare tukabahatika kutembelea la miti Silayo ambalo liko wilayani Chato mkoani Geita, ni shamba kubwa sana, ni shamba ambalo linatoa ujumbe wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ilivyodhamiria kuendeleza uhifadhi, na hapa nitafafanua baadae kidogo, kuna kitu nitakieleza kwanza ili twende sawa sawa.
Pamoja na kutembelea Shamba la Miti Silayo ambayo ndani yake pia kuna ufugaji nyuki, nikapata pia nafasi ya kutembelea hifadhi ya Msitu Rwamgasa iliyopo eneo la Nyarugusu, katika msitu huo Serikali kupitia Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania( TFS) imeamua kujenga kambi maalum kwa ajili ya watumishi wake kukaa karibu na kuulinda vema msitu huo ambao ulikuwa umebaribiwa na shughuli za kibinadamu.
Sikuishia hapo baadae nikatembelea kitalu kikuu cha miti ya michi kilichopo Geita, ni kitalu ambacho kinategemewa na Wana Geita kupata miche kwa ajili ya kupanda kwenye mashamba na maeneo ya wazi, hakika kuna kazi inafanywa na TFS , ni kazi kubwa na nzuri, hakika wanastahili pongezi.
Kwangu najihisi mwenye bahati kubwa, kweli kuishi kwingi kuona mengi, nimeona yanayofanywa na TFS katika utunzaji wa mazingira na uhifadhi sambamba na ulinzi wa utunzaji wa rasilimali za mazao yatokanayo na misitu yetu.
Kabla ya kuendelea na ninachotaka kukielezea kuhusu ziara yangu ya mikoa ya Kanda ya Ziwa na nilichokiona kwenye uhifadhi, naomba niielezee kidogo hii TFS , ni kuelezea tu ili uijue inafanya nini na kisha tuendelee.
Ni hivi Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania ulianzishwa kisheria kupitia Tangazo la Gazeti la Serikali (GN 269) la Julai 30, 2010 na kuzinduliwa rasmi Julai 18, 2011.
Kuanzishwa kwa TFS ni kwa mujibu wa Sheria ya Wakala “the Executive Agencies Act Cap. 245 (Revised Edition 2009)”, pamoja na Sera ya Misitu ya mwaka 1998, Sera ya Ufugaji Nyuki ya mwaka 1998, Sheria za Misitu na Nyuki Sura 323 na Sura 224 za mwaka 2002.
Aidha TFS iliundwa kwa kuzingatia Programu ya Serikali ya Maboresho katika Utumishi wa Umma ya mwaka 2000 (Public Service Reforms Programme (PSRP 2000)iliyolenga kuimarisha Idara na Wakala (Ministerial Departments & Agencies (MDAs)
Katika kuhakikisha utoaji wa huduma bora na madhubuti katika utumishi wa umma, ambapo Wakala zinakuwa na uwezo, motisha na mbinu za mabadiliko yenye kuleta ufanisi na tija kiutendaji.
Hata hivyo lengo Kuu la Kuanzishwa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania Kwa kuzingatia programu tajwa, Wakala wa Huduma za Misitu umeundwa kwa madhumuni ya kuhakikisha: Uwepo wa usimamizi madhubuti na wenye ufanisi na tija wa rasilimali za misitu na nyuki.
Pia kuongeza ubora na thamani ya kifedha katika kutoa huduma kwa umma; na kuendelea kukuza na kuboresha uwezo wa kutoa huduma kwa umma.
Katika muktadha huo masuala ya uendelezaji sera na sheria, pamoja na kanuni na taratibu zake yanashughuliwa na Idara ya Misitu na Nyuki katika Wizara ya Maliasili na Utalii. Hata hivyo majukumu ya Wakala yameongezeka licha ya kutoshughulikia sera na sheria.
Wakala umepanua wigo kibiashara na kuongeza maeneo ya uzalishaji miti na mazao ya nyuki ili kukidhi mahitaji halisi, shughuli za uwekezaji, kuboresha njia mbadala za mapato na uboreshaji wa hifadhi za misitu na nyuki kwa ujumla.
Kuhusu Dira ni Kuwa kielelezo bora katika usimamizi endelevu wa rasi…
Moja ya nyumba ya watumishi wa TFS iliyojengwa ndani ya Hifadhi ya Msitu Rwamgasa uliopo eneo la Nyarugusu mkoani Geita