Breaking

Saturday, 24 June 2023

MLOGANZILA YAJIPANGA KUKABILIANA NA MAGONJWA YASIYOAMBUKIZA KWA WATUMISHI WAKE

Hospitali ya Taifa Muhimbili Mloganzila imezindua Mloganzila Afya Jogging Club kwa lengo la kuhamasisha watumishi kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao na kukabiliana na magonjwa yasiyo ambukiza.

Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Club hiyo kwa niaba ya Naiba Mkurugenzi Mtandaji, Mkurugenzi Msaidia wa Rasilimali Watu na Utawala Bw. Abdalla Kiwanga amesema kuwa lengo la klabu hiyo kuwajenga na nikuwasaidia watumishi kufanya mazoezi kila mara ili kuimarisha afya zao na waweze kufanya kazi wakiwa imara.

“Sisi tumekuwa wasimamizi afya za watanzania lakini wakati mwingine tunajisahau kuwa na sisi tunatakiwa kuimarisha afya zetu ili tuendele kuwa vizuri na kuenedelea kuwasimamia watanzania na watu wengine kuwa na afya imara na waweze kujenga uchumi wa nchi.” Amesema Bw. Chiwanga

Vilevile amewapongeza watumishi wote waliojitokeza kufanya mazoezi na kuwataka waendelee kujitokeza kila wakati ili kuendelea kuimarisha Club hiyo na kuwa endelevu.

“Hichi tulichikifanya leo ni muhimu kwa afya zetu ,leo tumefungua rasmi clabu yetu ya Mloganzila Afya Jogging Club na tunataka club hii iwe hai hivyo nawasihi wote kwa pamoja tujenge utamaduni wa kukutana kila siku jioni na kila mwisho wa wiki tukimbie na kufanya mazoezi ili kuimarisha club yetu.Amesema Bw. Kiwanga

Mloganzila Afya Jogging Club imeanzishwa kwa lengo la kuunga mkono juhudu za wizara ya afya ya kuzuia na kupambana na magonjwa yasiyo ambukiza.


Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages