Mkuu wa Wilaya Mbinga Aziza Mangosongo akiambatana na kamati ya usamala ya usalama, wakuu wa taasisi na idara kutoka Halmashauri, alifanya ziara katika kijiji cha makongo tarafa ya hagati, kutatua mgogoro baina ya Mwenyekiti wa kijiji na wananchi baada ya kuwasilisha tuhuma dhidi yake. Sambamba na hilo alisikiliza na kutatua changamoto zingine zinazowakabili wananchi
Hatua hii inakuja kufuatia tuhuma na sababu zilizowasilisha na wananchi wa kijiji hicho wakimtaka *ndugu Joshua Lupogo* aliyekuwa Mwenyekiti wa kijiji kuondolewa madarakani kutokana na tuhuma za rushwa, Unyanyasaji sambamba na kuwabambikizia wananchi kesi na kufikishwa mahakamani pasipo sababu za msingi pamoja na matumizi mabaya ya ofisi.
Mkuu wa Wilaya mbinga Mhe. Mangosongo alieleza kwamba kumwondoa mwenyekiti madarakani kuna sheria na kanuni za kufuata kabla ya kumwondoa madarakani,Ambapo alimruhusu Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga*Jobu Mwalukosya* kueleza sheria hizo kwa wananchi kabla ya zoezi hilo.
Ambapo mwanasheria alieleza kwamba zipo sheria na kanuni za kufuatwa ambazo ni " Kumpata mwenyekiti wa muda, Kukidhi idadi ya wajumbe, Mwenykiti anayetuhumiwa kujibu tuhuma kwa kusomewa na mtendaji wa kijiji, wajumbe kupiga kura za siri, Hatua hizo zote zilifuatwa kwa mujibu wa kifungu cha 105 (3) cha sheria za serikali za mitaa, Mamlaka za Wilaya sura ya Na. 287 kadiri ya marekebisho ya 2002,Endapo mtuhumiwa atoridhika na maamuzi atapaswa kukata rufaa kwa Mkuu wa Mkoa ndani ya siku 30 kuanzia siku aliyotenguliwa kupinga maamuzi hayo.
Aidha, Mkuu Mkuu wa Wilaya alitangaza kuwa kuanzia 15/06/2023 *Ndugu Joshua Lupogo* aliyekuwa Mwenyekiti wa kijiji cha makongo kutenguliwa baada ya wananchi kupiga kura za hapana 212 kati ya kura za siri 275 za wajumbe wote kumwondoa madarakani, Hata hivyo aliwataka wananchi kuendelea kumpatia ushirikiano, kujali haki zake kwasababu huyo ni binadamu kama wengine, Vilevile alimtaka
kushiriki shughuli za maendeleo ndani ya kijiji
Sambamba na hilo, Mhe. Mangosongo Mkuu wa Wilaya Mbinga alipokea changamoto nyingine za wananchi ikiwemo ubovu wa miundombinu ya barabara na madarasa ya shule ya msingi, umeme n.k, Ambapo Mkuu wa Wilaya aliwahakikishia wananchi serikali chini ya *Mhe. Samia Suluhu Hassan*, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itazidi kuboresha huduma hizo ili kuchochea kasi ya Maendeleo na ukuaji wa uchumi.
Alikadhalika, Aliwataka wazazi kuchangia chakula ya wanafunzi shuleni, Kutowapatia vyombo vya usafiri watoto chini ya miaka 18, Kukemea tabia za ukatili wa kijinsia, Kutunza mazingira kwa kupanda miti, Kuhimiza watoto kwenda shule ili kuondoa changamoto ya utoro, Vilevile kusimamia maadili ya watoto.
Naye, Aliyekuwa Mwenyekiti wa kijiji Ndugu Joshua Lupogo baada ya kutenguliwa alisema "Nashukuru kwa ushirikiano mlionipatia kwa kipindi cha miaka mitatu, Pia Nitaendelea kushirikiana na wananchi na viongozi katika shughuli za Maendeleo kikubwa nisitengwe"
Mwisho, Naye Mwenyekiti wa muda *Ndugu Ansigary Mbungu*, alimshukuru Mheshimiwa Mkuu Wilaya kwa kusimamia vyema sheria na kanuni za nje zinavyopaswa, Vilevile alisema kwamba anaomba ushirikiano kutoka kwa wananchi na pale atakapokosea ataomba kushauriwa ili kutokwamisha shughuli za maendeleo ndani ya nje ya kijiji.
IMETOLEWA NA
OFISI YA MKUU WA WILAYA MBINGA
JUNI 15, MWAKA 2023