Breaking

Wednesday 14 June 2023

DAWASA KUSAJILI WATOA HUDUMA MAGARI YA MAJISAFI


Watumishi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) wamekutana na wasimamizi wa vizimba vya majisafi kwa ajili ya kupeana mwongozo wa zoezi la usajili wa magari ya utoaji huduma ya majisafi katika jiji la Dar es Salaam na Mkoa wa Pwani linalotarajia kufanyika kuanzia tarehe 19 hadi 30 Juni 2023.

Lengo la usajili huo ni kuratibu huduma ya majisafi kupitia magari na kuhakikisha huduma inayotolewa kwa wananchi ambao hawajafikiwa na miundombinu ya DAWASA inakidhi vigezo vilivyoweka na Mamlaka.



Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages