NA MWANDISHI WETU
WIZARA ya Maliasili na Utalii kwa kushirikiana na WWF imewakutanisha wadau mbalimbali kwaajili ya kujadili utekelezaji wa mkataba wa Kimataifa wa Biashara ya Wafanyamapori na mimea iliyo hatarini kutoweka .
Lengo la Warsha hiyo ni kuwashirikisha wadau muhimu wanaowajibika katika utekelezaji wa Mkataba wa “CITES” ili waweze kufahamu maamuzi yaliyotolewa katika mkutano wa 19 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa “CITES” uliokuwa umefanyika Jijini Panama.
Akizungumza wakati anafungua warsha hiyo leo Mei 9,2023 Jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori Dkt.Maurus Msuha amesema kupitia warsha hiyo itasaidia kuandaa mkakati wa pamoja wa utekelezaji wa maazimio ya mkutano pamoja na kujenga uwezo wa taasisi zinazotekeleza Mkataba wa “CITES” ili yale yanayoamuliwa kwenye mikutano ya Kimataifa utekelezaji wake uwe kwa njia rahisi hapa nchini.
Amesema Mkataba wa “CITES” umeweka mfumo wa utoaji maamuzi kuhusu utekelezaji wa Mkataba kuanzia ngazi ya Kamati za Kitaalam, Kamati Kuu na Mkutano wa Nchi Wanachama “Conference of Parties”.
Aidha amesema katika Mkutano wa 19 wa Nchi Wanachama wa Mkataba (CITES COP19) uliofanyika Jijini Panama ulijadili masuala ya kimkakati kuhusu biashara ya kimataifa ya wanyamapori na mimea iliyohatarini kutoweka, uwindaji wa kitalii, uhifadhi wa wanyamapori jamii ya tembo, simba, chui, faru, usimamizi na utunzaji wa shehena za meno ya tembo (Ivory stockpiles) na mchango wa uhifadhi kwa maendeleo ya jamii.
"Maamuzi ya mkutano huo yametoa mustakabali wa uhifadhi na biashara kwa takribani spishi 600 za wanyamapori na mimea". Amesema Dkt.Ombeni
Pamoja na hayo amesema ushiriki wa Tanzania katika CoP 19 umeleta manufaa makubwa katika uhifadhi na ustawi wa uwindaji wa kitalii kwa kuchaguliwa kuingia katika Kamati muhimu za uendeshaji wa Mkataba wa CITES (Kamati ya Wanyama, Kamati ya Mimea na Kamati Kuu na Kamati ya Bajeti na Mipango iliyochini ya Kamati Kuu).
Kwa upande wake Afisa Wanyamapori Bw.Elisante Ombeni amesema baada ya warsha hiyo watekelezaji wa mkataba huo, ambao ni Shirika la la Hifadhi za Taifa Tanzania (TANAPA), Mmalaka ya Usimamizi wa Wanayamapori Tanzania (TAWA), Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania(TFS), Taasisi ya Wanyamapori Tanzania (TAWIRI), (TAFIRI) watakuwa na ufahamu wa yale ambayowanapaswa kuyatekeleza.
Amesema warsha hiyo inamanufaa kwa wale wadau ambao hawajafikiwa kutambua ni mazao gani ya wanyamapori na misitu ambayo kwasasa yanaruhusiwa kufanyiwa biashara Kimataifa na mazao gani ambayo hayaruhusiwi pia na masharti ambayo yamewekwa kwa mujibu wa Mkataba wa “CITES” kwaajili ya kuwezesha biashara ya wanyamapori na Misitu inayolindwana Mkataba.
Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori Dkt.Maurus Msuha akifungua warsha ya kujadili utekelezaji wa mkataba wa Kimataifa wa Biashara ya Wafanyamapori na mimea iliyo hatarini kutoweka uliofanyika leo Mei 9, 2023 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori Dkt.Maurus Msuha akizungumza katika warsha ya kujadili utekelezaji wa mkataba wa Kimataifa wa Biashara ya Wafanyamapori na mimea iliyo hatarini kutoweka uliofanyika leo Mei 9, 2023 Jijini Dar es Salaam
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkaazi, WWF-Tanzania Dkt.Laurence Mbwambo akizungumza katika warsha ya kujadili utekelezaji wa mkataba wa Kimataifa wa Biashara ya Wafanyamapori na mimea iliyo hatarini kutoweka uliofanyika leo Mei 9, 2023 Jijini Dar es Salaam
Afisa Wanyamapori Bw.Elisante Ombeni akizungumza katika warsha ya kujadili utekelezaji wa mkataba wa Kimataifa wa Biashara ya Wafanyamapori na mimea iliyo hatarini kutoweka uliofanyika leo Mei 9, 2023 Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Idara ya Wanyamapori Dkt.Maurus Msuha (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na wadau mbalimbali katika warsha ya kujadili utekelezaji wa mkataba wa Kimataifa wa Biashara ya Wafanyamapori na mimea iliyo hatarini kutoweka uliofanyika leo Mei 9, 2023 Jijini Dar es Salaam
Wadau mbalimbali wakiwa katika warsha ya kujadili utekelezaji wa mkataba wa Kimataifa wa Biashara ya Wafanyamapori na mimea iliyo hatarini kutoweka uliofanyika leo Mei 9, 2023 Jijini Dar es Salaam
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)