Breaking

Thursday, 11 May 2023

UZINDUZI WA KAMATI YA UTALII TIBA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Mratibu wa matibabu nje ya nchi kutoka Wizara ya Afya Dkt. Asha Mahita amesema hospitali za kibingwa zinatakiwa kujenga uaminifu na ukarimu kwa wagonjwa wanaowahudumia ili kupunguza idadi ya wagonjwa wanaokwenda nje ya nchi kutibiwa kwani huduma zote za kibingwa sasa hupatikana hapa nchini.

Ameyasema hayo leo wakati wakati wa uzinduzi wa kamati za utalii tiba kutoka Hospitali za Taifa Muhimbili (MNH), Hospitali ya Mifupa Muhimbili (MOI)na Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency iliyopo jijini Dar es Salaam.
 

Amesema dhana ya utalii tiba nchini ilikuwa bado haijaeleweka vizuri hapo awali lakini tangu kuanza kwa kamati maalum ya utalii tiba mabadiliko makubwa yametokea kwani sasa wagonjwa kutoka nchi nyingi za Afrika wanakuja Tanzania kupata huduma za matibabu ya kibingwa yanayotolewa na Hospitali zetu.

Aidha amesema lengo kubwa la utalii tiba ni pamoja na kuongeza pato la nchi lakini pia mtu mmoja mmoja katika nchi kufaidika kupitia utalii tiba kwani wagonjwa wanaofika watahitaji malazi na huduma nyingine hivyo wote kwa pamoja kukuza uchumi wa nchi na uchumi binafsi.

“Kuzindua kamati za utalii tiba ni tukio kubwa katika sekta ya tiba utalii hapa nchini, nawapongeza kwa niaba ya Wizara kwa kazi kubwa ambayo kamati ya kitaifa ya utalii tiba imefanya tangu walipoteuliwa mwaka 2021 hadi sasa”, amesema Dkt. Asha

 Pamoja na hayo Dkt. Asha amezitaka Hospitali zote nchini kujitathmini na kuamua zinataka kufanya nini ili kuendana na malengo ya wizara inapojiandaa kutengeneza muongozo ambao utaleta majukumu ya kada zilizopo katika Hospitali kuwezesha kila mfanyakazi kuchukua nafasi yake na kutekeleza majukumu yake.

Naye Mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya utalii tiba Prof. Mohamed Janabi alisema kupitia kamati ya kitaifa ya utalii tiba wameweza kuujulisha umma nini maana ya utalii tiba hivyo kupunguza idadi ya watu waliokuwa wanakwenda nje ya nchi kwa ajili ya kupata huduma za matibabu.

Prof. Janabi ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili alisema kufikia mwaka 2030 Tanzania inatarajia kuwa na watalii milioni tano waonafika hapa nchini kwa mwaka na kupitia watalii hao wapo baadhi ambao watahitaji huduma za matibabu hivyo ni vyema Hospitali zikaendelea kuboresha huduma na kuvitunza vizuri vifaa tiba kwani ni vya gharama.

“Dhumuni letu kubwa kama kamati tunataka tupate angalau asilimia 10 ya wagonjwa wanaokwenda nchi za ulaya kwaajili ya matibabu kutibiwa katika nchi yetu kwasababu sasa vifaa tunavyo na wataalam kwaajili ya kutoa huduma za kibingwa wapo wakutosha”, alisema Prof. Janabi.



Mratibu wa matibabu nje ya nchi kutoka Wizara ya Afya Dkt. Asha Mahita akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge kitabu chanye mpango mkakati wa utalii tiba kilichoandaliwa na kamati wa kitaifa ya utalii tiba leo wakati wa uzinduzi wa kamati za utalii tiba kutoka Hospitali za Taifa Muhimbili (MNH), Hospitali ya Mifupa Muhimbili (MOI)na Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mratibu wa matibabu nje ya nchi kutoka Wizara ya Afya Dkt. Asha Mahita akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Ocean Road Dkt Julius Mwaiselage kitabu chanye mpango mkakati wa utalii tiba kilichoandaliwa na kamati wa kitaifa ya utalii tiba leo wakati wa uzinduzi wa kamati za utalii tiba kutoka Hospitali za Taifa Muhimbili (MNH), Hospitali ya Mifupa Muhimbili (MOI)na Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency iliyopo jijini Dar es Salaam.


Mratibu wa matibabu nje ya nchi kutoka Wizara ya Afya Dkt. Asha Mahita akimkabidhi Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge kitabu chanye mpango mkakati wa utalii tiba kilichoandaliwa na kamati wa kitaifa ya utalii tiba leo wakati wa uzinduzi wa kamati za utalii tiba kutoka Hospitali za Taifa Muhimbili (MNH), Hospitali ya Mifupa Muhimbili (MOI)na Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa matibabu nje ya nchi kutoka Wizara ya Afya Dkt. Asha Mahita akimkabidhi Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dkt.Lemeri Mchome kitabu chanye mpango mkakati wa utalii tiba kilichoandaliwa na kamati wa kitaifa ya utalii tiba leo wakati wa uzinduzi wa kamati za utalii tiba kutoka Hospitali za Taifa Muhimbili (MNH), Hospitali ya Mifupa Muhimbili (MOI)na Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) uliofanyika katika Hoteli ya Hyatt Regency iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mratibu wa matibabu nje ya nchi kutoka Wizara ya Afya Dkt. Asha Mahita akizungumza wakati wa uzinduzi wa kamati za utalii tiba kutoka Hospitali za Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Mifupa Muhimbili (MOI), na Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) uliofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa kamati ya kitaifa ya utalii tiba Prof. Mohamed Janabi akizungumza wakati wa uzinduzi wa kamati za utalii tiba kutoka Hospitali za Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Mifupa Muhimbili (MOI), na Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) uliofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency iliyopo jijini Dar es Salaam.

Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) Dkt. Peter Kisenge akizungumza wakati wa uzinduzi wa kamati za utalii tiba kutoka Hospitali za Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Mifupa Muhimbili (MOI), na Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) uliofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency iliyopo jijini Dar es Salaam.


Mkurugenzi Mtendaji wa Ocean Road Dkt Julius Mwaiselage akizungumza wakati wa uzinduzi wa kamati za utalii tiba kutoka Hospitali za Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Mifupa Muhimbili (MOI), na Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) uliofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency iliyopo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Mifupa Muhimbili (MOI), Dkt.Lemeri Mchome akizungumza wakati wa uzinduzi wa kamati za utalii tiba kutoka Hospitali za Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Mifupa Muhimbili (MOI), na Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) uliofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency iliyopo jijini Dar es Salaam.
Wanakamati wa utalii tiba wakifuatilia haflaya uzinduzi wa kamati za utalii tiba kutoka Hospitali za Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Mifupa Muhimbili (MOI), na Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) uliofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency iliyopo jijini Dar es Salaam.

Wanakamati wa utalii tiba wakipata picha ya pamoja na Mratibu wa matibabu nje ya nchi kutoka Wizara ya Afya Dkt. Asha Mahita wakati wa uzinduzi wa kamati za utalii tiba kutoka Hospitali za Taifa Muhimbili (MNH), Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI), Hospitali ya Mifupa Muhimbili (MOI), na Taasisi ya Saratani Ocean Road (ORCI) uliofanyika leo katika Hoteli ya Hyatt Regency iliyopo jijini Dar es Salaam.

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages