Breaking

Tuesday, 16 May 2023

TUKIO LA PANDA 2023 KUKUTANISHA WASICHANA WAJASIRIAMALI KUJADILI UJUZI WA KIDIJITALI KWA BIASHARA ENDELEVU


Wajasiriamali wa kike nchini wanatarajiwa kukusanyika katika hafla ya Panda 2023 Mei 12, iliyoandaliwa na shirika la Her Initiative kushirikiana na Ubalozi wa Uholanzi, UN-women, Women Fund Tanzania, NCBA, EFM na DUMA- Jumuiya ya Masoko ya Chuo Kikuu cha es -Salaam. Tukio hili linalenga kusherehekea mafanikio ya jukwaa la Panda Digital na kuunda mjadala juu ya "Ujuzi wa Dijitili kwa Biashara ya Endelevu."

 

Kupitia shirika la Her Initiative, vijana wanawake nchini Tanzania wanawezeshwa kwa maarifa, ujuzi, na rasilimali ili kuzalisha kipato chao wenyewe kuondokana  na umaskini na kuwa uhuru wa kifedha. Tangu kuzinduliwa kwake mwaka wa 2021, jukwaa la Panda Digital limetoa ujuzi kwa wajasiriamali vijana wanawake  zaidi ya 5,000 kupitia matumizi ya tovuti na muundo wa SMS.

Tukio la Panda ni jukwaa la kutambua mchango wa wajasiriamali vijana wanawake kwa uchumi wa kitaifa na kujadili masuala yanayohusu matumizi ya uvumbuzi na teknolojia katika kubadilisha biashara zisizo za kidigitali kuwa biashara za digital. Tukio hili linalenga kuwaandalia vijana wanamke  mazingira wezeshi kutengeneza ustawi wa kiuchumi wa kidijitali na kukuza mbinu za kukabiliana na udhalilishaji au ubaguzi wa kijinsia yanayoathiri ujumuishaji wa wasichana katika uchumi wa kidijitali kwa. Kupitia mjadala wa jopo na maonyesho ya kisanii, Panda Event 2023 inalenga kuunganisha mgawanyiko wa kidijitali wa kijinsia na kukuza teknolojia ambayo inayozingatia mahitaji ya wanawake.

Panda Event 2023 ni jukwaa moja  wapo la wajasiriamali wa kike nchini Tanzania kujifunza, kuboresha ujuzi, mtandao, na kupata fursa kama vile mitaji na masoko. Tukio hili ni njia ya mazungumzo na kujenga sauti ya pamoja ambayo inachangia kuunda mazingira wezeshi kwa vijana wa kike kustawi katika uchumi wa kidijitali.

 

Lydia Charles Moyo, Mkurugenzi wa Her Initiative, vjana wanawakeJukwaa la Panda Digital limebadilisha maisha ya vijana wajasiriamali wa kike nchini Tanzania, "Kupitia Panda Event, idadi kubwa ya wasichana na vjana wanawake watafikiwa.

Asha Hemed mnufaika wa jukwaa la Panda" , amenukuliwa akisema, "Kabla sijajua kuhusu Panda Digital, biashara yangu ilikuwa ndogo na haina uhai, hivyo basi  haikufanikiwa kama nilivyotegeme, lakini yote hayo yalibadilika baada ya kujua kuhusu Panda Digital".

  

ZINGATIO KWA WAHARIRI

Panda Event 2023 ni fursa kwa vijana wanawake wajasiriamali nchini Tanzania kuunganishwa, kubadilishana uzoefu, na kujenga mitandao itakayowawezesha kustawi katika uchumi wa kidijitali.

 

Her Initiative ni shirika linaloongozwa na vjana wanawake, ambo huboresha thamani ya wasichana na kuunda kanuni mpya kwa kuvunja mzunguko wa umaskini na kujenga uwezo wa kifedha miongoni mwa wasichana na vijana wanawake nchini Tanzania. Program na miradi yetu huwapa wasichana maarifa, ujuzi na kuwaunganisha na rasilimali ili kuwasaidia kuzalisha mapato yao wenyewe. Kupitia kazi yetu, tunahimiza ushiriki wa wasichana na vijana wanawake katika shughuli za kuzalisha kipato ili kufikia usawa wa kijinsia na ukuaji wa uchumi jumuishi.

 

Anwani P.O BOX 66

Her-Initiative

Simu: 25573428334

Barua pepe: info@herinitiative.or.tz

Mtandao: www.herinitiative.or.tz



Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages