Breaking

Wednesday, 3 May 2023

TGNP WASHAURIWA KUWAJENGEA UWEZO VIONGOZI WA SERIKALI ZA MITAA

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

MTANDAO wa Jinsia Tanzania TGNP wameshauriwa kuweka nguvu kubwa kuwajengea uwezo viongozi wa Serikali za Mitaa hasa wenyeviti ili wajue wajibu wao, kujua namna ya kusimamia bajeti, kujua namna ya kuwashirikisha wananchi kuibua miradi ya maendeleo pamoja na kusimamia utekelezaji wa bajeti.

Ushauri huo umetolewa leo Mei 3, 2023 na washiriki wa Semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) Jijini Dar es Salaam, Semina ambazo hufanyika kila Jumatano na kukutanisha wadau mbalimbali ambao mara nyingi hushiriki Semina hizo ambazo huandaliwa na TGNP Mtandao.

Akizungumza katika semina hiyo, Mwezeshaji wa Semina za Jinsia TGNP, Bw.Deogratius Temba amesema katika Semina hiyo Jamii imekuja na maadhimio ya kwamba inahitajika semina zaidi zifanyike kwenye ngazi ya Serikali za Mtaa na wakaona kuna mapungufu makubwa kwenye uelewa yaani viongozi wa Serikali za Mitaa hasa wenyeviti na watendaji hawafahamu majukumu yao ipasavyo.

Amesema baada ya Semina hiyo wanategemea kuona wananchi wakienda kushirikiana na viongozi wao zaidi katika kutekeleza bajeti ambayo inapitishwa na kwenda kushiriki vizuri katika mchakato wa uandaaji wa bajeti ngazi ya msingi na kutoa maoni yao.

"Wananchiwamepata uelewa mpana na wanazidi kujiongezea maarifa kuhusu mamlaka za Serikali za Mitaa na namna Serikali hiyo inavyoendeshwa na kuweza kushirikiana vizuri wa wenyeviti pamoja na watendaji wa mitaa". Amesema Bw.Temba.

Kwa upande wa washiriki wa Semina hiyo wamesema kupitia semina hiyo wamejifunza mambo mengi ikiwemo kutambua majukumu ya kila kiongozi katika Serikali za mitaa na namna ya kufanya ikitokea kiongozi hajatekeleza majukumu yake.

Amesema tutegemee mabadiliko ya kifikra kwenye jamii katikautekelezajiwa majukumya kiongozi kwenye ngazi ya Serikalli za Mitaa na kuweza kufahamu ni namna gani tunaweza kupata kiongozi bora ambaye anaweza kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
Mwezeshaji wa Semina za Jinsia TGNP, Bw.Deogratius Temba akiendesha semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) leo Mei 3,2023 Jijini Dar es Salaam, Semina ambazo hufanyika kila Jumatano na kukutanisha wadau mbalimbali ambao mara nyingi hushiriki Semina hizo ambazo huandaliwa na TGNP Mtandao.

Mwezeshaji wa Semina za Jinsia TGNP, Bw.Deogratius Temba akiendesha semina za Jinsia na Maendeleo (GDSS) leo Mei 3,2023 Jijini Dar es Salaam, Semina ambazo hufanyika kila Jumatano na kukutanisha wadau mbalimbali ambao mara nyingi hushiriki Semina hizo ambazo huandaliwa na TGNP Mtandao.

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages