Na Mwandishi Wetu
MJUMBE wa Halmashauri Kuu (NEC) ya Chama Cha Mapinduzi( CCM) Salim Abri Asas amesikitishwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa wakimtukana matusi kwa sababu ameamua kuisaidia jamii ya watu wa chini.
Pamoja na kushambuliwa huko bado amewaambia wananchi kwamba ataendelea kusaidiana na kushirikiana nao na hafanyi hivyo kwasababu za kiasa kwani hana mpango wa kugombea ubunge bali anasaidia kwa sababu za kuona anayo nafasi ya kufanya hivyo.
Akizungumza na kundi la wafanyabiashara wadogo wadogo (Machinga)katika Manispaa ya Iringa ambao mwezi Machi mwaka huu waliamishwa katikati ya Mji na kutengewa eneo la Mlandege kwa ajili ya kuendesha shughuli zao,
Asas ametumia nafasi hiyo kuelezea masikitiko yake kutokana na kuandamwa na baadhi ya wanasiasa.
"Lazima mnielewe nawafikishieni ujumbe , lazima muelewe bila kumung'unya maneno , kuna watu wanakerwa sana na mimi kuwasaidia ninyi , watu wakiona nimekuja kusaidia natukanwa matusi.
"Kuna chama kimoja kimenitukana , wamenisema ajenda ni mimi baada ya kufuatilia wanasema wamekereka kwasababu nawasaidia ninyi Machinga , yaani kweli mimi nisimsaidie huyu mama, nikimsaidia wewe unakereka , nikimsaidia muuza samaki unakereka?
"Waniseme , wanitukane, wanibeze , wanikere mimi sitoacha kuwasaidia mama zangu, dada zangu.Sijawahi kuuliza mtu chama chake .Kwanini mtu asaidie watu anakereka?Amehoj Asas wakati anazungumza na Machinga hao ambao baadhi ya walisikika wakitaja wanasiasa wanamshambulia Mjumbe huyo wa NEC
Kuhusu changamoto za wamachinga hao, Asas ametumia nafasi hiyo kuahidi kuendelea kuwasaidia na kushirikiana nao ili kutatua kwa kutatua changamoto mbalimbali kama vile ukosefu wa umeme, maji, mitaji kufa kwa baadhi ya wafanyabiara.
Katika kutatua hayo Asas ameutaka Uongozi wa shirikisho la Machinga kupeleka gharama zote hadi kufanikisha kuwekwa kwa umeme na maji katika eneo hilo pia amewaahidi kuwapatia Mtaji kwa ajili ya kunusuru biashara zao.
Ikumbukwe si mara ya kwanza Asas kusaidia kundi hili kwani aliwaikuwachangia Sh. Milioni 100, ambapo Sh Milioni 50 zilitumika kuboresha miundombinu ya kufanyia biashara zao na Sh.milioni 50 nyingine kwa ajili ya mfuko wao.