Breaking

Tuesday, 16 May 2023

MWANAFUNZI WA KIDATO CHA NNE AUAWA KWA KUCHOMWA KISU NA MWENZAKE



Mwanafunzi wa kidato cha nne katika Shule ya Sekondari ya Faza nchini Kenya, ameaga dunia baada ya kudaiwa kudungwa kisu na mwenzake wakati wakicheza.

Siku ya Jumatatu, Mei 15, Citizen Digital iliripoti kwamba mwanafunzi huyo wa miaka 18, alikabiliana na mwenzake mwenye umri wa miaka 17 wa kidato cha tatu katika shule hiyo wakati wa 'breaktime'. 

Ugomvi wao uligeuka na kuwa mauti baada ya mshukiwa ambaye alitoroka kumdunga kisu mwenzake mgongoni. 

Mwanafunzi huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Faza Level 4 Hospitali akiwa hali mahututi, ila alitangazwa kufariki alipowasili hapo. 

Abud Mohamed, mzee wa kijiji, alithibitisha mkasa huo na kuwataka wenyeji kuwa na utulivu huku polisi wakimsaka mshukiwa.

 “Ilianza na kugombana kidogo na kuanza kurushiana cheche za amneno.Ghafla mambo yakawa mabaya na mmoja wao kupandwa na hasira na kumdunga kisu mwenzake,” Abud alisema. 

Mwalimu mkuu wa shule aliyetambulika kama Shoka, alithibitisha ripoti hizo ila akasema hakuwa shuleni wakti kisa hicho kilipotokea. 

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages