Breaking

Friday, 26 May 2023

MWALIMU AMBAKA MWANAFUNZI WAKE KISHA AMPA SHILINGI ELFU 10




Mahakama ya Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa, imemuhukumu kifungo cha Miaka 30 Jela Mwalimu Onesmo John Sanga (51) wa Shule ya Sekondari Kibengu iliyopo wilayani hapa baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka mwanafunzi wake  na kumpatia ujauzito (17).


Kesi hiyo ya jinai namba 28 ya mwaka 2023 ambayo hukumu yake imetolewa Mei 23, 2023  na Hakimu Mkazi Mwandamizi wa Mahakama hiyo Benedict Nkomola. 


Sanga alitenda kosa hilo Februari 12 na Novemba 6, 2022 huko maeneo ya  Kijiji cha Kibengu, K ata ya Usokame Wilaya Mufindi kwa kutenda kosa hilo huku Mahakama ikamtia hatiani kwa makosa mawili ya ubakaji chini ya kifungu cha sheria 130 (1)(2)(e) na 131 (1) cha kanuni ya adhabu sura ya 16 rejeo la Mwaka 2022.


Aidha ilielezwa mahakamani hapo, mshtakiwa alikuwa akimdanganya Mwanafunzi huyo kwa kumpatia fedha ya Sh10,000 baada ya kumfanyia ubakaji huo huku akimwahidi kumsaidia katika masomo yake.


Inadaiwa kuwa sababu ambayo imepelekea mshtakiwa kufikishwa mahakamani hapo ni baada ya mwalimu huyo kumpa ujauzito mwanafunzi wa wa kidato cha tatu wa shule hiyo hali ambayo ilisababisha mwanafunzi huo kuumwa baada ya kupewa dawa kwa ajili ya kutoa ujauzito huo.


Hata hivyo mahakama hiyo imetoa adhabu ya kifungo cha miaka 30 jela ambapo adhabu hiyo itaenda sambamba kwa makosa yote mawili huku ikitoa amri kwa mshtakiwa kumlipa fidia ya Sh5 milioni mwathirika huyo..../


Via: Mwananchi



Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia langolahabari@gmail.com au WhatsaApp: +255 621 896 990

Pages